Wafungwa wote katika jela ya Barwon mjini Victoria wanahitajika kufanya kazi isipokuwa wanapokuwa wagonjwa sana ama wakati wanapokuwa wazee sana .Wafungwa waliogoma wanasema kuwa dola 6.90 walizoahidiwa katika makubaliano mapya hazitoshi kusimamia gharama yao ya maisha.Upinzani nchini humo unataka walazimishwe kurudi kufanya kazi ,ukisema kuwa wananchi wamekasirishwa na hatua kwamba wafungwa hao wana uwezo wa kugoma.Malipo ya dola 9 kwa siku ambayo wafungwa hao wameahidiwa ,kulingana na kazi zao na saa wanazofanya kazi ,ni ongezeko la malipo ya sasa ya kati ya dola 6.50 na dola 8.95,lakini imekosolewa kutotosha na wafungwa na wafuasi wao.Malipo hayo ni ya kiwango cha chini sana ikilinganishwa na majimbo mengine nchini Australia na hayafikii gharama zao zinazoongezeka kila uchao,alisema Brett Collins,msemaji wa kundi linalopigania haki za wafungwa.
Source BBC
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment