Mjadala huu pia uligusia mapenzi na pesa, nitaelezea baadaye walivyosema wachangiaji mbalimbali.Mjadala mkubwa ulikuwa ukiuliza `ni mapenzi gani yana raha zaidi yakifanyika kati ya wale waliopo ndani ya ndoa au wale waliopo nje ya ndoa?’
Pia iliongezwa hoja kuwa unapofanya mapenzi na `nyumba ndogo’ unapata raha zaidi kuliko unapofanya mapenzi na mkeo ndani ya nyumba’Hoja hii ilipingwa sana na akina mama wengi, ingawaje wengi wa akina baba walisema ni kweli ukiiba nje ya ndoa unafaidi zaidi, na starehe yake si sawa na unapofanya na mkeo.
Sababu kubwa wengine walisema ni kama chakula ulichokizoea huwezi ukakilinganisha ni kile unachokipata kwa nadra. Wengine walidai ni udhaifu wa wake zetu ambao hawajitumi, tofauti na yule wa nje ambaye analifanya lile penzi ili umpende zaidi.
Na akina mama waliokubali hili walisema inasababishwa na akina baba ambao penzi lao zuri walilitoa tu siku ile ya `fungate’ baada ya hapo huchoka kuliendeleza kwa tamaa zao na ndio maana ukimpata mume nje unafaidi zaidi kwa vile analifanya lile penzi kwa hamasa na mvuto wa aina yake.
Sasa je wewe kama Dada Dinah, au na wachangiaji wengine ambao huenda mna uzoefu wa yote mawili, kuwa mliwahi kuyafanya mapenzi mkiwa nje ya ndoa na pia mumewahi kuyafanya mkiwa ndani, au mliwahi hata kuiba nje ya ndoa, je ni kweli tofauti ipo na kwanini iwepo, na tufanyeje ili kuiondoa tofauti hiyo? Au nyote mnasema `nyama ni ileile hata ukiipika vipi’.
emu-three.
Jawabu: Asante M3, Mimi binafsi sina uzoefu huo kwa sababu kuu 2, kimaadili,kiimani na kiutu sitoweza kufanya hivyo na pili, ni kuwa maisha yangu ya kingono na mwenzangu yana afya, tunatamaiana kama ndio tumekutana sasa hivi!
Hakuna uhusiano kati ya wizi na kufurahia mapenzi, ikiwa mtu anafurahia au kuhisi utamu wa mapenzi ya wizi basi atakuwa na matatizo yake binafsi ya Kisaikolojia.
Ni kama wale wanaofurahia kufanya mapenzi zaidi ikiwa wanajua kuna watu wanawaangali au baadhi wenye kupenda kupiga "chabo" kwamba hanyegeki mpaka akachungulie watu wengine wakifanya mambo fulani au wale wenye matatizo ya kiakili na kujikuta wanapenda kufanya ngono na watoto wadogo au ajuza.
Ili kufurahia mapenzi na kuhisi ni matamu mnahiaji mapenzi kati yenu, Uwazi wa nini mnataka,ubunifu nakujituma kwenu wote wawili, ufanyaji wa mhusika na ile hali ya kuvutiwa/tamanisha.
Mmoja wenu akijisahau hapo basi maisha yenu ya kingono yana kuwa hatarini na unaweza usitamani tena kufanya ngono na mkeo/mumeo na ikitokea mnafanya inakuwa wajibu zaidi(kupunguza nyege kwa vile huna pa kwenda kuzipunguzia) kuliko mapenzi.
Natambua kuna swala la wanaume na wanawake kuchepuka na hilo linasababishwa na vjimambo na vijisababu ambavyo nilishawahi kuvizungumzia kwenye Makala za nyuma.
Nini cha kufanya ili kuondoa uwezekano wa wapenzi kuchepuka nje ya ndoa:-
1-Kurudisha thamani ya ndoa.
2-Kuheshimu wenza wetu.
3-Kutojisahau mara tu baada ya kufunga ndoa/kuzaa.
4-Kuboresha mawasiliano na yawe kwa uwazi zaidi.
5-Kuboresha utendaji wenu kwa ushirikiano zaidi.
6-Kutochukulia wanawake kama kiburudisho cha ngono.
7-Kujifunza na kujaribu mambo mapya kila siku.
8-Kuhakikisha "romance" inabaki pamoja na kuwa wewe na yeye ni mama na baba sasa.
9-Fahamu/tambua uhusiano wenu ume-base kwenye nini na boresha zaidi hapo.
10-Kufanya mambo pamoja kama wapenzi na sio baba na mama fulani (peleka watoto kwa bibi yao ili kuwa na wakati wenu kama zamani).
NB: Pamoja na mambo mengine ni muhimu sana kujuwa uwezo wa kingono wa mpenzi wako kabla hajawa wa "milele" ili kuepuka michepuko. Ukijua mapema inakuwa rahisi kwako kujua kama utaweza kumudu na kama hutoweza kumudu basi utajitolea mhanga kuvumilia au kutafuta mbunu m-badala za kuridhishana.
Natumaini nimejibu kama ulivyotarajia, kama hujaridhika niambie kipengere gani nikiongelee kwa mapana na marefu!
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment