Umeshawahi kusikia utete wa kuibiana nyimbo baina ya mastaa wa Bongo Fleva? Ni ishu inayokua kila siku huku baadhi ya mastaa wakidaiwa kunufaika kwa nyimbo au mistari ya kuiga au kuiba. Je, ni visa gani vya kuigiana idea au kuibiana nyimbo vimewahi kutokea Bongo?
Tazama
Sugu vs Mr Blue ‘FREEDOM’
Mr. Blue a.k.a Byser alitoa ngoma FREEDOM aliyomshirikisha Sugu lakini siku chahche baadae Sugu nae akatoa ngoma yenye jina hilo hilo ‘FREEDOM’ lakini ikiwa haina sauti ya Mr. Blue na akatoa na video ya ngoma hiyo. Blue akalalamika kuibiwa nyimbo lakini Sugu akatumia kipindi cha luninga na kumtumia prodyuza Master Jay kueleza kilichotokea na kwanini ni haki yake kumiliki ngoma hiyo.
Dully Sykes vs Nuhu Mziwanda ‘INDE’
Tofauti na kesi ya Mr. Blue na Sugu, Nuhu Mziwanda amedai kuibiwa ‘wazo’ la ngoma ya Dully Sykes ‘INDE’. Dully amejibu nini kuhusu tuhuma hizo? Dully Sykes amedai kuwa wazo la nyimbo hiyo sio la kwake bali alipewa na Harmonize na yeye alichokifanya ni kuliboresha.
Q Chief vs Soprano ‘TUSHAONANA WABAYA’
Shaaban Katwila a.k.a Q Chief au Chillah aliwahi kuingia kwenye maneno na staa mwingine wa Bongo Fleva, Soprano na tatizo lilikuwa ngoma ‘Tushaonana wabaya’.
Soprano alidai kuwa ngoma hiyo ilikuwa yak wake na alimshirikisha wazo na mistari ya ngoma yake ‘TUSHAONANA WABAYA’ Q Chief lakini baadae staa huyo (Q Chief) akaja na ngoma iliyokimbiza sana ‘TUTAONANA WABAYA’.
Hbaba vs Diamond ‘NATAKA KULEWA’
Unaikumbuka ngoma iliyompa Diamond Platnumz mileage kubwa miongoni mwa ngoma zake? Ilikuwa ngoma NATAKA KULEWA. Ilikuwa ikihusishwa na uhusiano wake na mastaa kadhaa wa Bongo akiwemo aliyekuwa mpenzio wake, Wema Sepetu. Diamond baada ya KUTAKA KULEWA, staa mwenzake nae kwenye Bongo Fleva, H-Baba akaja na lalamiko kuwa nyimbo hiyo ni wazo lake na Diamond Platnumz aliiba wakiwa studio.
Jay Moe vs Mwana FA ‘KAMA UNATAKA DEMU vs MI NA MABINTI’
Ni ngoma ambazo zimeshabihiana sana kwa mashairi na ladha huku zote zikiwasifu wanawake mbalimbali mastaa wa Bongo. Nani alimuiga mwenzake? Jay-Moe ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa ngoma KAMA UNATAKA DEMU na baadae FA akaja na MIMI NA MABINTI DAMU DAMU.
Tetesi zilizagaa kuwa FA amekopi idea ya Jay Moe lakini kwa hekima kubwa suala la kufanana kwa ngoma hizo likamalizwa bila kumuingiza hatiani yeyote kati yao.
Kuiga au kuiba ngoma ya mwenzako kunaashiria nini? Au waliolalamika walikuwa wanatafuta kiki?
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment