Kulegea kwa misuli ya uke ni hali ya mama kulegewa na pelvic organs zake kama mlango wa uzazi,urethra, au mfumo wa kutolea mkojo (bladder) na kumfanya kutokuwa kwenye hali ya kawaida,uke unatanuka kwa ndani.
Kulegea kwa uke wa mwanamke kupo kwa aina tofauti
Prolapse of bladder -kuta za uke za mbele zinapolegea (prolapse of bladder) zinamsababishia mwanamke kushindwa kuhimilia kubana kibofu cha mkojo na kujikuta mkojo unatoka bila kujijua wakati wa kukohoa,kupiga chafya au akiwa anafanya mazoezi.
Enterocele-misuli ya uke inapolegea sababu ya mishipa ya mbele na nyuma ya uke inajitenga ina kuja kusababisha misuli yote ya kulegea kutokukaza.
Kulegea kwa mishipa ya uterus.
Hili tatizo la kulegea kwa mishipa ya ukeni inawapata wanawake wengi wakifika kwenye umri mkubwa kipindi cha (menopause) na wengine wanapata kipindi cha kujifungua mtoto ( childbirth).Wanawake wengi wanaona aibu kwenda hospital kuomba ushauria ua tiba wanakaa kimya tu .
Sababu zinazosababisha kulegea kwa uke
Childbirth-mama anapojifungua ikawa amejifungua kwa complations nyingi inachangia kuharibu tissue ,misuli za ukeni na kuchangia kulegea
Multiple birth-mama mtoto zaidi ya mmoja yani mapacha 2,3,4 na kuendelea wanauwezo wa kulegea kwa misuli ila kumbuka sio kila mama hapo inategema kila mtu na mwili wake ,wengine wanaweza zaa mapacha na misuli ya uke isilegee.
Menopause ostrogen-ni hormones anazokuwa nazo kila mwanamke zinasaidia kuafanya pelvic organs zake kiwe na nguvu zaidi ,ila mwanamke anapofikisha miaka 40-50 zile hormones zinapungua kuzalishwa na ndio hapo mwanamke anapata tatizo la kulegea kwa misuli ya uke.
Umri mkubwa -wanawake wenye umri miaka 50 na kuendelea wanahatari ya kulegea kwa misuli.
Uzito mkubwa-mwanamke mnene anaweza pata tatizo la kulegea kwa uke
Wanawake wengine wanazaliwa tayari wakiwa na mapungufu haya ya kulegea kwa uke
Kuzaa kwa karibu karibu -watoto kupishana umri mdogo sana kunasababisha misuli ya uke kulegea
.kusukuma mtoto kwa muda mrefu sana
• Ukubwa wa mtoto
• Kuchanwa au kuchanika sana wakati wa kujifungua• Ama mtoto alivutwa wakati wa kutoka
Dalili ya kulegea kwa misuli ya uke
Mwanamke atahisi kama kuna nyama iyiootea kwa nje na kuning’inia au kwa ndani na inazuia kidole kuingia wakati wa kujisafisha kwa wale wanaotumia vidole
Kutokusikia hamu ya tendo la ndoa,kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kutokwa maji maji na kupata michubuko
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Maumivu ya mgongo
Kutokwa damu ukeni bila siku zako kufika
swala lote la uzazi kibiologia linaleta athari katika mfumo mzima wa uzazi hasa sehemu za (ukeni) .kujifungua kwa kawaida au c-section (operation) kunaweza leta complication na kufanya raha ya mapenzi isiwepo.
Wakati mwanamke anapata uchungu /kujifungua kuruhusu kichwa kupita nje ya mji wa mimba kwa kupitia uke . hatua hii huweza kusababisha mikwaruzo, kuvimba na maumivu katika ukuta wa uke
Athari za matatizo hayo yanaleta kuondokewa na hisia za kimapenzi au mama kupata maumivu makali akikutana kimwili.
Na swala la kutokutana kimwili huleta athari zingine ambazo hupelekea mahusiano kuwa mabaya zaidi. Mwanamke anaanza kutojiamini, anajinyanyapaa, hariziki na tendo la ndoa na mwisho ugomvi ama kutoka nje ya ndoa.
Nini kifanyike:
mwanamke ambaye anahisi kuna utofauti kabla na baada ya kujifungua. Kwanza jaribu kuingiza vidole viwili visafi vilichooshwa na maji safi na sabuni ingiza sehemu za siri kama vinapita kwa urahisi jua uke umeongezeka zimepanuka , weka viwe vitatu ukiona vinaongia bila tatizo weka na cha nne nacho kikapita jua umepata tatizo la kutanuka kwa misuli ya ukeni ,na iwapo umeweka kidole cha kwanza na kimepita kwa shida basi huna tatizo upo salama uke wako upo size ile ile ya kawaida.
Tiba ya kulegea kwa misuli ya uke
Matibabu yake yapo mama akiona dalili hizo hapo juu basi anatakiwa kwenda hospital kumwona daktari wa magonjwa ya wanawake kumwangalia tatizo lake lipoje kuna baadhi ya vipimo atachukuliwa ,mwanamke anaweza fanyiwa upasuaji wa kurekebisha misuli au kupatiwa dawa itategemea na hali aliyonayo.Iwapo ukafanyiwa upasuaji hutakiwa fanya tendo la ndoa mpaka kidonda kipone baada ya wiki 4-6 usipofanya hivyo ni rahisi kupata infection.
Mazoezi nayo yanasaidia misuli ya kuta za uke kukaza na kufanya uke urudi kwenye size ya kawaida na wapenzi kufurahia tena tendo la ndoa mazoezi haya ni kama ifutayo
Fatilia iyo picha hapo juu kunja mguu mmoja na mwingine kunjua na shika vidole vya miguu huku mkono mwingine ukiwa kwenye mguu fanya mara 2 kwa siku kwa dakika 15-20
• Jaribu kubana misuli ya uke kwakubana miguu , bana pumzi ndani na kaza misuli ya mbele na sehemu ya haja kubwa hii itasaidia kubana misuli ile iliyolegea fanya mara kwa mara uwezavyo.
• Pili jaribu kujisaidia haja ndogo kwa kituo hii pia husaidia kubana misuli ya uke
Mazoezi haya husaidia kubana misuli ya kibofu cha mkojo, njia ya haja kubwa, kizazi na njia ya mkojo.
mazoezi haya huweza pia kusaidia wanawake wenye matatizo kama ifuatavyo
➢ watu ambao mkojo unatoka bila kujizuia wakipiga chafya, kukohoa ama kucheka
➢ wanasikia hamu ya kukojoa gafla kila mara.
Ushauri
Kumbuka kuzaa haraka haraka bila watoto kupishana ni hatari kwa afya yako,ukipata magonjwa ya infections wahi hospital yote hayo yana fanya misuli ilegee. Iwapo unatatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke usione aibu kwenda hospital linatibika na utafurahia tena tendo la ndoa na mpenzio
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment