KOCHA WA VINCENT BOSSOU ANUSURIKA KIFUNGO GEREZANI,ALIMWA FAINI


Strasbourg,Ufaransa.

KOCHA wa timu ya taifa ya Togo inayochezewa na beki kisiki wa Yanga,Vincent Bossou,Mfaransa Claude LeRoy amenusurika kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kufanya udanganyifu katika masuala ya usajili wa wachezaji wakati akiifundisha klabu ya Racing Club de Strasbourg ya Ufaransa mwanzoni mwa miaka ya 1990 na 2000.

Mapema mwaka huu Leroy,68, pamoja na Rais wa Racing Club de Strasbourg,Patrick Proisy,walikutwa na hatia ya kufanya udanganyifu katika sajili za wachezaji wanne tofauti.

Wachezaji hao ni golikipa wa zamani wa Paraguay,Jose Luis Chilavert, Mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa,Peguy Luyindula.Mshambuliaji wa zamani wa Senegal,Henri Camara na Per Pedersen wa Denmark.

Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema LeRoy ameamuliwa na mahakama kuu ya mji wa Strasbourg kulipa faini ya Euro 15,000 (£12,790).

Wakati LeRoy akikumbana na faini hiyo aliyekuwa mshirika wake wakati huo Rais wa zamani wa Racing Club de Strasbourg,Patrick Proisy,nae amelimwa faini ya Euro 25,000 (£21,340) sambamba na kupewa kifungo cha miezi kumi gerezani ambacho hata kitumikia kwa sasa.Mtuhumiwa wa tatu katika kesi hiyo,Nicolas Geiger,wakala wa zamani wa wachezaji yeye amekumbana na faini ya Euro 4,000 (£3,415).



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: