Michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea tena hapo kesho kwa michezo minne kupigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
African Lyon ikipambana na Azam FC, katka mechi ya ligi kuu msimu huu
Mkurugenzi wa ufundi wa African Lyon ambayo hapo kesho itacheza dhidi ya JKT Ruvu, Charles Otieno amesema, mchezo uliopita dhidi ya Yanga ambao walipoteza kwa bao 3-0 ulikuwa mgumu kutokana na vijana kushindwa kuelewa mfumo lakini wanaamini mara baada ya kucheza mechi nyingi watakuwa sawa kwa ajili ya kuweza kupata pointi tatu kwa kila mechi.
Otieno amesema, mechi za mwanzoni ni muhimu kupata pointi tatu ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri na hakuna timu inayojipanga kwa ajili ya kupata sare au kufungwa katika mechi kwani kila timu inahitaji kujiweka katika nafasi za juu zaidi.
Otieno amesema, wamewaangalia JKT Ruvu katika mchezo wao dhidi ya Simba na wameshafanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika michezo miwili iliyopita hivyo wanachosubiri kwa sasa ni dakika tisini katika mchezo wa hapo kesho.
Otieno amesema, kikosi kitashuka hapo kesho kikiwa kamili na hakuna majeruhi hivyo wanaamini wataweza kuchukua pointi tatu Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani.
Michezo itakayopigwa hapo kesho ni African Lyon itakayokuwa ugenini dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani, Mbao FC ikiikaribisha Mbeya City uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Kagera Sugar ikiikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera huku Majimaji akimkaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Majimaji Mkoani Ruvuma
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment