Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imewafungiwa wachezaji watano kutoka klabu tano zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas
Kwa mujibu wa ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema Shirikisho limetoa tahadhari kwa klabu za Mbeya City, Majimaji, Mwadui FC, Mbao FC na African Lyon kutowatumia wachezaji hao, kwani watatu wamefungiwa mwaka mmoja na wawili wamesimamishwa kwa juma moja.
“Mchezaji George Mpole wa Majimaji amefungiwa mwaka mmoja kwa kudanganya jina na kujiita Gerard Mpole, alikuwa anatumia akiwa Kimondo FC, Wiliam Lucian “Galas wa Mwadui akitokea Ndanda FC na Said Mkopi aliyesajiliwa na Mbeya City akitokea Tanzania Prisons”, alisema Lucas.
Pia Lucas alisema wachezaji Emanuel Kichiba aliyesajiliwa na Mbao FC na Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon wamepewa juma moja kuwasiliana na timu zao za zamani ambayo ni Ashanti United ili kukamilisha taratibu za uhamisho.
Lucas alisema wachezaji hao wamegundulika kufanya udanganyifu huo kupitia usajili ambao wamefanya hapo awali kwani sura za kwenye picha ni ile ile, lakini majina ndio yamebadilishwa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment