Serena Williams atupwa nje michuano ya Olimpiki



Nyota namba moja wa mchezo wa tenisi duniani, Serena Williams ametupwa nje ya mashindano ya michezo ya Olimpiki baada ya kushindwa na mchezaji wa Ukraine Elina Sitoniva katika hatua ya tatu ya tenisi ya mashindano ya wanawake.
Nyota namba moja wa mchezo wa tenisi duniani, Serena Williams.
Bingwa huyo wa dunia alionekana kufanya makosa mara tano mfululizo katika raundi ya saba kipindi cha pili.
Serena ameshindwa kwa seti 6-4, 6-3 na Elina ambaye anashika nafasi ya 20 duniani.
Aidha Serema alisema kuwa haikuwa kama alivyotarajia lakini siyo mbaya sana kwasababu angalau alifuzu kushiriki michuano hiyo ya Rio Olimpiki.
"Haikuwa kama nilivyokuwa nataka iwe lakini angalau nimeweza kufuzu kuja Rio, hilo lilikuwa kati ya malengo yangu, mchezaji mzuri leo ameshinda lakini najua kuwa wakati mwingine utakuwa mchezo mzuri sana na nasubiri wakati huo"- alisema Serena Williams
William na mdogo wake Venus wametolewa katika mashindano ya wawili siku ya Jumapili na raia wa Jamhuri ya Czech, Lucie Safarova na Barbora Strycova.





Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: