MAAJABU!!!! DEREVA ASIYE NA MIKONO ADAKWA NA POLISI AKIENDESHA GARI


Wo Guo akiwa ndani ya gari lake
Wo Guo akiwa ndani ya gari lake
Polisi nchini China wamemkamata mtu asiyekuwa na mikono akiendesha gari.  Bwana huyo Wo Guo (45) si tu kwamba hakuwa na leseni bali alikuwa akitumia mguu wake wa kulia kubadili gia huku mguu wa kushoto ukikanyaga mafuta na breki.
Msemaji wa polisi amesema: “Ni jambo la ajabu, lakini ni hatari sana kwake kuendesha gari.” Polisi huyo amesema itakuwa vyema kama ataajiri dereva wa kumuendesha. Gari la bwana Wo linashikiliwa na polisi ili kumzuia asiendelee kuendesha.
Bwana 'Wo Guo' akimuonyesha askari aliyemkamata namna anavyoingiza gia
Bwana ‘Wo Guo’ akimuonyesha askari aliyemkamata namna anavyoingiza gia

 akisomewa shitaka lake
Wo Guo akisomewa tuhuma na Askari wa usalama Barabarani



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: