LIGI KUU BARA:AZAM FC YABANWA MBAVU NYUMBANI NA AFRICAN LYON


Dar Es Salaam,Tanzania.
AZAM FC imebanwa mbavu nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na African Lyon katika mchezo safi na mgumu uliomalizika usiku huu katika uwanja wa Chamazi,Mbagala-Dar Es Salaam.
African Lyon ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 46 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Hood Abdul Mayanja kwenda moja kwa moja langoni.
Mpira ukiwa unaelekea ukingoni mashabiki wakiwa wamekata tamaa,John Bocco "Adebayor",aliisawazishia bao Azam FC dakika ya 93 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Salum Abubakar Sure Boy na kufanya mchezo kuisha kwa sare ya bao 1-1.
Vikosi
Azam FC:Aishi Manula,Ismail Gambo/Mudathir Yahya,Bruce Kangwa,
Himid Mao, David Mwantika,Jean Mugiraneza, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/
Francesco Zekumbariwa,Shomary Kapombe,Frank Domayo/Kipre Balou,John Bocco na Shaaban Idd.
Afrcan Lyon;Youthe Rostand, Baraka Jaffar,Khalfan Twenye, Hamad
Waziri, William Otone, Omar Salum, Hamad Manzi,Mussa Nampaka, Omar
Abdallah/Abdul Hilal,Hood Mayanja na Tito Okello.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: