KABILA LAKO.KUMBE WAMAKONDE WANAOGOPA KUFA...!




Inaelezwa kwamba Maziko Wamakonde huwa na maombi tofauti na yale yanayofuatwa na madhehebu mengine. Badala ya Sheikh au Kasisi kusoma dua, Wamakonde wana desturi ya kuieleza maiti maombi na maonyo ili marehemu huyo asije patwa na madhara wala asiandamwe na mikasa katika safari yake huko aendako, na pia ndugu wanaobaki nyuma wasikabiliwe na mabalaa na mikosi ya aina yoyote. Wenyewe wanaamini kwamba mabalaa huongozana, yaani likitokea moja hufuata la pili, la tatu na kadhalika. Kwa mujibu wa simulizi zao, kuna madai kwamba pale mambo hayo ya mila yanapopuuzwa vifo mfululizo hutokea katika familia husika.

Mkuu wa mazishi Huieleza maiti wakati wa maziko:

“Ndugu umeacha jembe, mshale, shoka, nyumba na kazi kwa hiyari yako mwenyewe, hakuna aliyekulazimisha kufunga safari hii, ile wewe mwenyewe umeazimia. Umetuacha sisi huku nyuma kwa hiyari yako mwenyewe, Hivi, ufikapo kwenye ukomo wa safari yako, ukaeleze yanayokuhusu wewe binafsi.Wakikuuliza  ‘Wako wanadamu wengine waliobaki?’ ukawajibu, ‘hapana.’ Ujitahidi kuwathibitishia kwamba ni wewe tu peke yako, hakuna mtu mwingine aliyebaki.”

Kwa maneno hayo, inadhihirisha wazi kabisa kwamba waliobai nyuma wanaogopa kufa. Ingawa wanajua kuwa kufa kupo, ila kama kunaweza kukwepeka basi ombi lao lisikilizwe! 

Hata hivyo inadaiwa kwamba mila hii bado inafuatwa na Wamakonde wa Msumbiji, tofauti na Wamakonde wa Tanzania ambao mila kwa kiasi kikubwa zimeathiriwa  muingiliano wa makabila na dini hizi za mapokeo


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: