1- Kamwe usisahau kumuomba Mungu wako kabla hujasema “YES” kwa yule unaedhani anapaswa kujenga maisha na wewe. Usikimbilie kuolewa. Kama utakimbilia kuolewa, utaikimbia ndoa na tena kwa majeraha makubwa.
2- Tambua lengo lako kabla hujaingia kwenye ndoa. Fanya biashara yoyote, tafuta shughuli ya kufanya. Usimsubiri mwanaume ndio useme unaanza maisha. Ongeza thamani ya maisha yako kwa kujenga maisha yako.
3- Usimkimbilie mwanaume kwa sababu ya pesa zake, magari, connection, cheo, kipaji, ucheshi, au background ya familia yake. Olewa na mwanaume aliye na hofu ya Mungu. Hapo utakua umekula BINGO…!
4- Jenga tabia ya kula vizuri kwa afya. Usile alimradi umekula. Kula vyakula vya kujenga mwili na uwe mlo kamili. Fanya mazoezi mara kwa mara kuepuka unene usio wa lazima.
5- Vaa vizuri. “first impression counts” hii inamaanisha kwamba muonekano wa mwanzo unamaana sana kwa mtu atakayekuona. Usiache maeneo yako ya siri yakaonwa na mwanaume yeyote, vinginevyo utawavutia wale wanaume wakware ambao sio waoaji.
6- Usililie au kulazimisha mwanaume akuoe. Wewe ni wa thamani mno kufanya hivyo. Usilazimishe ndoa kwa kumbebea mimba, wenzako wamefanya hivyo na leo wengi wao wanajuta. Wamebaki wakilea peke yao.
7- Tabia yako ndio Ndoa yako. Hiyo ndio itakayoamua mwanaume aishi na wewe au laa. Jitathimini tabia yako. Uzuri sio kila kitu, kama unajivunia na uzuri wako na unaamini kama ndio utakaokupa mume utapoteza nafasi yako kwa aliye mzuri zaidi yako kwa tabia na sura.
8- Usichoke kujifunza kupika, kujua kupika wali, ugali, mboga na chapati haitoshi. Jifunze zaidi, tizama vipindi vya mapishi, soma vitabu mbalimbali vya mapishi, tembelea page mbalimbali zinazofundisha kupika vyakula aina mbalimbali.
Wanaume mara nyingi wanapenda wanawake wanaojua kupika, wale ambao kila siku wana suprise ya aina mpya ya mapishi. Kwa sababu njia nyingine rahisi ya kutambua moyo wa mwanaume ni kupitia tumbo lake (chakula kizuri)
9- Usiishi kwa mazoea utakapoolewa, soma vitabu vya mahusiano, ndoa na familia. Ongea na wazazi wako na wazee wengine wakupe busara zao. Kupitia kwao akili itaweza kupanuka na kupata ufahamu wa nani haswa atapaswa kuishi na wewe.
10- Acha ushabiki kwenye mitandao ya kijamii mambo ya Team Zari, Team Wema, Team Chura, na mengineyo hayatakusaidia. Wenzako wana maisha yao, muda huo tumia kuhudhuria semina mbalimbali za ndoa, tembelea washauri wa mahusiano na ndoa.
Msome Chriss Mauki, Tweve Hezron, Eliado Tarimo, Prince Naahjum Alsina na wengineo kwa dondoo mbalimbali za mahusiano, kupitia huko ufahamu wako waweza kuongezeka kwa kiasi fulani, hii itaepusha sana kuja kuishi kwa mazoea.
******************
Ni hayo tu sina la ziada, Binafsi wanawake nawakubali sana, sijui kwanini…!? labda kupitia ujasiri wa mama yangu. Ninafahamu kupitia ninyi tunaweza tukawa na familia bora ambako huko ndiko maadili ya taifa huanzia.
Heshima ya mwanamke ni NDOA, heshima ya mwanaume ni MAJUKUMU.
Life is full of joy, Enjoy it!
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment