HENRY AULA KWAO NA LUKAKU, HAZARD.




henry
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal ambaye pia alikuwa akifanya kazi kama mchambuzi wa masuala ya soka kwenye kituo cha televisheni cha Skysports ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa nchi ya Ubelgiji chini ya Roberto Martinez.
Henry hivyo ataenda kutengeneza jopo la makocha pamoja na Graeme Jones, ambaye alikuwa msaidizi wa Martinez kule Swansea, Wigan na Everton.
Henry alisema “najsikia mwenye furaha kubwa na ninajisikia vyema kuchaguliwa kushika nafasi hii. Namshukuru Roberto Martinez na pia chama cha soka cha nchini Ubelgiji. Nina furaha sana, na sitaki kungoja”.
Martinez alisema “Thierryni mtu wa muhimu sana na ataleta kitu kikubwa na cha msingi sana kwenye kikosi chetu. Ni vyema sana kuwa nae”.
“Henry ni mtu anayejua kutengeneza akili sahihi na muono unaotakiwa kwa wachezaji, namna ya kufanya kazi pamoja na kushinda. Alitwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998 huku pia akiwa na uzoefu wa kushinda mambo mengi.”
Henry anategemewa kuongeza uzoefu wake kwenye vichwa vya washambuliaji wengi waliokuwa katika kikosi cha Ubelgiji kama Romelu Lukaku, Christian Benteke, Divock Origi, Michy Batshuayi na Kevin De Bruyne.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: