UJENZI WA CHUO CHA VETA LUDEWA

Na Barnabas Njenjema Ludewa,
Juhudi za Serikali Ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli Kwakushirikiana na Mbunge Wa Jimbo la Ludewa Mh. Deo Ngalawa za kuhakikisha Chuo cha Ufundi Stard VETA Chenye hadhi ya Mkoa Kinajengwa katika Kijiji cha Shaurimoyo Wilayani Ludewa Mkoani Njombe  Zimeanza Kuzaa Matunda Baada ya naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya Kufanya ziara ya Kutembelea na Kulikagua eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi Wa Chuo hicho kikubwa Huko Shaurimoyo Wilayani Ludewa.

Siku ya Jana Naibu waziri huyo Wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Injinia Stella Manyanya Amefanya Ziara hiyo ya Siku moja wilayani Ludewa katika Mkoa Wa Njombe akitokea Mkoani Ruvuma kisha Akapokelewa Na Mbunge Wa Ludewa Mh. Deo Ngalawa Pamoja na Mkuu Wa wilaya ya Ludewa Mh. Andrea Sere aliyeambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Ludewa Kisha Naibu waziri Akapelekwa Katika eneo la Ujenzi huo Wa Chuo Cha VETA shaurimoyo.
Akitoa Maelezo Juu ya Eneo hilo lililotengwa na wananchi kwa Ajili ya Ujenzi Wa Chuo hicho mbele ya Naibu waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Afisa Mipango miji na Vijiji wilaya ya Ludewa Bw. Izack Makinda amesema kuwa wananchi Wa kijiji cha Shaurimoyo walikubali kutenga Eneo lenye ukubwa Wa Ekari 78 kwaajili ya Ujenzi huo ambapo hadi sasa Mchoro Wa Ramani ya Ujenzi Huo umekamilika Tayari kwakuanza Ujenzi Wa Chuo hicho.

Suzana Magani ni Kaimu mkurugenzi Wa VETA kanda ya Nyanda za juu kwa Mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma Amesema kuwa Ujenzi Wa Chuo hicho unatarajia kuanza mwanzoni mwa  mwezi Wa 9 mwaka huu Huku Akiweka wazi Baadhi ya Fani zitakazotolewa Chuoni hapo.

Mara baada ya kupokea Maelezo hayo ya Utangulizi kutoka kwa Wataalamu mbalimbali Naibu waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Injinia Stella Manyanya Akazungumza kwakusema kuwa Uwepo Wa Chuo hicho wilayani Ludewa ni muhimu kwakuwa kitaweza kuzalisha Utaalamu kwa Vijana ambao watapata Fulsa ya Kufanya kazi katika Migodi mikubwa ya Madini ya  Chuma cha Liganga na Makaa ya mawe Nchuchuma wilayani Ludewa Huku akiwaagiza VETA kuhakikisha Ujenzi huo unaanza Maramoja Bila kutoa Sababu za Michakato kuendelea.

Mh. Deo Ngalawa ni Mbunge Wa jimbo la Ludewa kwa niaba ya wananchi akazungumzia Ujio huo Wa Chuo Kikubwa cha VETA Shaurimoyo Kuwa ni Chuo ambacho kitakuwa na Ubora Wa juu katika mkoa Wa Njombe hivyo anaamini wananchi wake wamelipokea kwa moyo Wa Amani jambo hilo jema pia pesa tayari ipo ya ujenzi huo.

Baadhi ya wananchi nao wakasema Ujio Wa chuo hicho wanaupokea kwa Furaha kubwa kwani ni Miaka mingi sasa imepita walikuwa wakipewa ahadi kuwa Chuo cha VETA kitajengwa Shaurimoyo hivyo kwasasa wanaamini Chuo hicho hakitachelewa ili vijana wao waweze kupata Taaluma ya Ufundi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: