50.1K
Reads
68
Comments
NYOTA wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo sasa ni kati ya wanamichezo wanne wanaoongoza kwa kuingiza fedha duniani, wakizidiwa tu mwanamuziki Taylor Swift, Boyband One Direction na James Patterson.
Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes ambalo limesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anaingiza kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 88 kwa msimu.
Kiasi hicho kinamuweka juu ya mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona anayeingiza dola Milioni 81.5 katika nafasi ya pili na nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James anayeingiza dola Milioni 77 katika nafasi ya tatu.

Namba | Muhusika | Pato lake |
1. | Taylor Swift | Dola Milioni 170 |
2. | One Direction | Dola Milioni 110 |
3. | James Patterson | Dola Milioni 95 |
=4. | Cristiano Ronaldo | Dola Milioni 88 |
=4. | Dr. Phil McGraw | Dola Milioni 88 |
6. | Kevin Hart | Dola Milioni 87.5 |
7. | Howard Stern | Dola Milioni 85 |
8. | Lionel Messi | Dola Milioni 81.5 |
9. | Adele | Dola Milioni 80.5 |
10. | Rush Limbaugh | Dola Milioni 79 |
Kwa mujibu wa Forbes, Ronaldo anapata Dola Milioni 55 kutokana na mshahara tu, wakati fedha nyingine zinatokana na mikataba yake ya udhamini.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United anafanya kazi na makampuni ya Nike, TAG Heuer, Sacoor Brothers Suits na Monster.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United anafanya kazi na makampuni ya Nike, TAG Heuer, Sacoor Brothers Suits na Monster.
Si ajabu Mreno huyo kuongoza sasa kwa kipato hivi sasa, ikiwa hata uwanjani ameendelea kufanya vizuri na mwaka huu ukiingia katika moja ya miaka ya kukumb ukwa kwenye maisha yake ya soka.
Shaun Botterill/Getty Images
Mei mwaka huu alifunga penalti ya ushindi dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Atletico Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya wiki iliyopita kuiongoza Ureno kutwaa taji la Euro 2016 wakiwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika fainali.
Ludewa yetu na maendeleo yetu