MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA MH:DEO NGALAWA AWAHAMASISHA WANANCHI KUUNDA VIKUNDI.
Baadhi ya vinu vya mashine ambazo vikundi mbalimbali wilayani Ludewa vimewezeshwa na Mh.Deo Ngalawa
Hizi ni motor za mashine hizo
Mashine zikishushwa ndani ya gari
Bw.Vasco Mgimba akichimba mtalo wa bomba za maji kutoka Ludende kuelekea Maholong'wa
katibu wa mbunge Bw.Fotunatus Fungatwende na Afisa wa ofisi ya Mbunge Bw.Victor Sanga wakishiri katika uchimbaji na ujenzi wa chanzo cha maji Ludende
mtungi wa gesi ambao ulinunuliwa na Mh.Ngalawa mbunge wa jimbo la Ludewa
hizo ndizo dawa zilizonunuliwa na Mbunge zikiwa katika zahanati ya Maholong'wa
Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh:Deo Ngalawa amewataka wananchi wilayani Ludewa kuunda vikundi ili kuweza kunufaika na fulsa zinazozitokeza hasa mikopo kwani bado wananchi wilayani hapa hawana utamaduni wa kuunda vikundi hali inayowafanya kujikita katika wimbi la umasikini.
Hayo yamesemwa jana na katibu wa mbunge huyo Bw.Fotunatus Fungatwende wakati akipokea mashine za kusaga,kukoboa na kukamua mafuta ya alizeti zilizotolewa na Mh:Ngalawa zikiwa na lengo la kuvigawia vikundi mbalimbali ambavyo viliomba kwa mbunge huyo.
Bw.Fungatwende alisema kuwa Mh.Ngalawa anamalengo makubwa ya kuinua uchumi wa wapiga kura wake lakini hataweza kutoa msaada kwa mtu mmoja mmoja lakini atatoa kwa vikundi ambavyo vimeundwa na wananchi wenyewe wakiwa na lengo kujiinua kiuchumi.
Alisema kuwa huo ni mwanzo tu kwa vikundi vilivyoundwa awali katika kata mbalimbali lakini ataendelea kutoa vitu mbalimbali katika vikundi ili wananchi waweze kuwa na miradi endelevu itakayowasaidia kujiinua kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo jamii itanufaika na miradi hiyo na anaamini itakuwa endelevu tofauti na kumuwezesha mtu mmoja mmoja.
Bw.Fungatwende alisema kuwa Mh.Mbunge wa jimbo la Ludewa ameona fulsa nyingi ambazo zinaweza kuwa vyanzo vya mapato kwa wananchi wa Ludewa lakini wakitaka kunufaika na fulsa hizo ni kujiunga katika vikundi na kuibua miradi yenye tija katika jamii nay eye kama mbunge wao atawaunga mkono katika juhudi hizo.
“Mashine hizi zinakwenda katika kata na vijiji mbalimbali katika wilaya ya Ludewa na tutazigawa kutokana na maombi ya vikundi husika hivyo Mh.Mbunge ameshauri wananchi kuendelea kuunda vikundi na kuibua miradi yeye kama mbunge wao atawaunga mkono,mpango uliopo ni mkubwa ili kukuza uchumi Ludewa na hauwezi kukamilika kwa kumsaidia mmoja mmoja hivyo ni vyema kutumia fulsa hii maana wengine ndio wameanza kunufaika kupitia vikundi”,alisema Bw.Fungatwende.
Katika hatua nyingine katibu huyo wa Mbunge aliweza kumuwakirisha Mh.Ngalawa katika uchimbaji wa mtaro wa bomba ilikufanikisha maji safi na salama yanapatikana katika kata ya Ludende kijiji cha Maholong’wa ambako awali aliweza kununua mtungi wa gesi katika zahanati ya kijiji hicho ili kuweza kupasha moto vifaa tiba.
Zahanati hiyo ya kijiji cha Maholong’wa kata ya Ludende wilayani hapa imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mtungi wa gesi pamoja na jiko lake pamoja na dawa za kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa muda mrefu hali iliyomlazim mbunge huyo kuvinunua vitu hivyo pamoja na dawa na kuukabidhi uongozi wa kijiji hicho.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment