UVCCM Yataka Majipu Ndani ya Chama Yaanze Kujitumbua ......Ni wale Waliokisaliti Chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka Jana


 ;
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Shaka Hamduni Shaka amewataka wanachama wanaojitambua kuwa ni majipu kwa kukisaliti chama kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana, waanze kujitumbua kabla hawajatumbuliwa.

Shaka alitoa rai hiyo jana katika mji wa Orkesumet na Kata ya Ngorika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakati wa ziara yake ya kuhamasisha vijana kujiunga na chama hicho, kufungua matawi mapya, kumsimika kamanda wa Kata ya Naisinyai na kukagua uhai wa chama.

Alisema lazima wajenge chama chenye heshima na nidhamu kuliko kuwa na wanachama wasaliti ambao hawana msimamo.

Shaka alisema wanachama wa aina hiyo nyakati za asubuhi wanakuwa sehemu moja na ikifika jioni wanakwenda kwingine.

“Ni heri wabakie wanachama wawili waadilifu kuliko wengi ambao hawana msimamo, kufanya kosa siyo kosa, bali kosa kurudia kosa, tunajua uchaguzi ukirudiwa tena hapa Simanjiro CCM itafanikiwa kushinda,” alisema Shaka.

Alisema kukata tamaa ni mwiko ukiwa CCM, kwa kuwa miaka mitano siyo mingi, hivyo wanatarajia kurudisha kata sita na Jimbo la Simanjiro linaloshikiliwa na Chadema.

Alisema hilo litafanikiwa kutokana na uongozi bora wa Rais John Mafuguli.

“Tumesikia wapo waliotusaliti wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tutawachukulia hatua, ila hivi sasa kutokana na juhudi za Rais Magufuli hata upinzani watatupigia kura za ndiyo,” alisema.

Mwenyekiti wa UVCCM, Wilayani Simanjiro, Kiria Laizer alisema vijana ndiyo nguvu ya chama, hivyo kupitia jumuiya hiyo wamejipanga kukipigania na kukitetea. 

“Vijana ndiyo nguzo ya chama, tumejipanga vizuri kuhakikisha kupitia CCM, wananchi wa eneo hili wanaendelea kukiamini na kukithamini, hivyo tutasonga mbele,” alisema



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: