NJIA 60 ZA KUMFURAHISHA MUMEO.





Katika mada yangu ya “njia 60 za kumfurahisha mkeo” niliahidi kuendelea na maudhui hii kwa kuwaletea mada ya “kumfurahisha mumeo”. Natangulisha shukrani kwa wale walioniandikia katika E-mail yangu na kupitia WhatsApp. Ifuatayo ni mada husika:

1. Anaporudi kutoka kazini, safarini au kwenye shughuli yoyote iliyowatengenisha, anza kwa salamu nzuri.
2. Unapompokea au kukutana naye basi fanya hivyo ukiwa na uso wa bashasha.
3. Vaa mavazi nadhifu. Jipambe na upake manukato kwa ajili yake.
4. Unapoanza kuzungumza naye anza na mambo au taarifa nzuri, na kama kuna taarifa mbaya subiri mpaka atakapopumzika.
5. Mpokee kwa maneno ya upendo na lugha ya kumpongeza au kumpa pole au lugha yoyote inayoonesha kumhurumia kwa kazi za kutwa nzima.
6. Ipendezeshe na uilainishe sauti yako kwa ajili ya mumeo… usifanye hivyo mbele ya wanaume wengine.
7. Utunze mwili wako na kujiweka katika hali ya umaridadi na siha njema.
8. Oga mara kwa mara, na pia baada ya siku zako.
9. Epuka kuwa katika hali ya uchafu au muonekano mbaya.
10. Epuka mapambo yaliyoharamishwa kama vile kujichora tattoo na kadhalika.
11. Tumia manukato, rangi na mavazi yanayopendelewa na mumeo.

12. Jitahidi mara kwa mara kubadili mtindo wa nywele, manukato na kadhalika. Lakini usizidishe kiwango, na ufanye hivyo kwa mumeo tu au mbele ya mahram wako.

13. Usichelewe kumpa mahaba pindi mumeo anapojiwa na hisia ya kutaka kufanya mapenzi.

14. Mwambie maneno matamu na yenye mvuto wa mahaba.
15. Ridhika na yale uliyoruzukiwa na kukadiriwa na Allah.
16. Kumbuka kuwa utajiri wa kweli hupatikana katika imani na uchamungu.

17. Usihuzunike kwa sababu mumeo ni masikini au anafanya kazi ya kawaida. Watazame maskini, wagonjwa na walemavu kisha umshukuru Allah kwa aliyowajaalia.

18. Usimuombe mumeo mambo mengi yasiyokuwa na ulazima.

19. Uchamungu hauna maana ya kutofurahia mambo mazuri nay a halali, bali una maana ya kuiangalia Akhera na kuyatumia yale uliyojaaliwa na Allah kwa lengo la kuifikia Pepo Yake.

20. Mshajiishe na umhamasishe mumeo kupunguza matumizi na kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya sadaka na kuwasaidia maskini na wale wenye dhiki.
21. Kuwa mwenye shukrani kwa mumeo.
22. Ukiwa mwenye shukrani, mumeo atazidi kukupenda na atajitahidi kukufurahisha na kukuridhisha zaidi.

23. Ukiwa mtovu wa shukrani, mumeo atasikitishwa na hali hiyo na kuanza kujiuliza: “Kwa nini nimfanye mambo mazuri mtu asiyekuwa na shukrani?” Epuka hali hiyo.

24. Daima kuwa mtiifu kwake.

25. Shikamana na mumeo, hususan katika nyakati za shida, dhiki, maradhi au mumeo anapofilisika au anapokuwa hana pesa.

26. Muunge mkono kupitia kazi yako, fedha yako au mali yako pindi inapohitajika.
27. Fuata maagizo yake, isipokuwa katika mambo ya haramu. Katika Uislamu, mume ni kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

28. Jaribu kuepuka yale yanayomkasirisha.
29. Mfurahishe anapokuwa ameghadhibika.
30. Ukimkosea muombe msamaha.

31. Akikosea usihamaki kwa kumfokea au kuzozana naye. Subiri anapokuwa hana ghadhabu na uzungumze naye kwa amani na kwa kauli nzuri.

32. Akiwa na hasira kutokana na mambo ya nje ya nyumba basi subiri mpaka atakapoondokana na hasira hiyo.

33. Mpe faraja na kumuonea huruma, yumkini akawa amechoka, ana matatizo ya kikazi au kuna mtu kamtusi, n.k.

34. Usimuulize maswali mengi au kung’ang’ania kutaka kujua yaliyotokea. Mathalan, kuna wanawake wengine wakiona mume ana hali tofauti huanza kusema: Niambie kumetokea nini? Lazima utaniambia kilichokufanya mpaka ukawa na hasira hivyo… unaficha nini? Nina haki ya kujua au kuna mwanamke kakuvuruga?

35. Jilinde dhidi ya mahusiano yaliyoharamishwa.

36. Tunza siri za familia, hususan mambo ya chumbani na mambo mengine ambayo mumeo hapendi watu wayajue.

37. Usisahau kushughulikia vizuri malezi ya watoto na huduma za nyumbani. Mumeo atafurahia kula chakula ulichompikia na chenye virutubisho.

38. Zilinde mali na fedha zake.
39. Usiende matembezini au nje ya maeneo ya nyumbani bila idhini yake; unapotoka vaa mavazi sahihi.

40. Usiwakaribishe au kukutana na watu ambao hapendi ukutane nao.
41. Usikae faragha na mwanaume yeyote ambaye sio mahram wako.
42. Kuwa mwema kwa wazazi na ndugu zake. Wakaribishe wageni wake.
43. Jitahidi sana kuepuka migogoro na ndugu zake.
44. Epuka kumuweka katika hali na mazingira ambayo anatakiwa kuchagua kati ya mamaye na mkewe.

45. Onesha ukarimu kwa wageni wake kwa kuwaandalia sehemu nzuri ya kukaa, chakula kizuri n.k.
46. Mhamasishe kuwatembelea ndugu zake nawe uwaalike kuja nyumbani kwako.

47. Wapigie simu wazazi wake na dada zake, watumie ujumbe mbalimbali wa kuwajulia hali, wanunulie zawadi, waunge mkono katika nyakati za matatizo na shida.
48. Usifuatilie au kutengeneza shaka zisizokuwa na msingi.
49. Wivu ni alama ya upendo wa mke kwa mumewe lakini usivuke mipaka ikafikia hatua ukawatukana watu au kuwavunjia heshima.

50. Kuwa mwenye subira na stahmala mnapokuwa katika wakati mgumu kifedha au kimaisha. Kuwa mvumilivu mnapokutwa na majanga mbalimbali na hususan mumeo anapofukuzwa kazi, mpe nguvu.

51. Shirikiana na mumeo na umkumbushe kutekeleza ibada mbalimbali za faradhi na za sunna.

52. Mhamasishe kuswali swala za usiku. Sikiliza na usome Qur’an Tukufu unapokuwa peke yako na ukiwa na mumeo pia. Mdhukuru Allah sana, hususan baada ya swala ya Alfajr na kabla ya Maghrib.

53. Jifunze sheria mbalimbali za Kiislamu na adabu za wanawake.
54. Msaidie mumeo katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kumpa nguvu,
kumhamasisha, kumpa ushauri mzuri, kumfariji na kadhalika.

55. Jitahidi nyumba iwe safi, ipanmbe na kuiweka katika mpangilio na mandhari mazuri.

56. Andaa chakula kizuri na kinachojenga afya.
57. Jifunze stadi zote muhimu za kuendesha nyumba kama vile ushonaji, mapishi na kadhalika.

58. Jifunze namna ya kuwalea watoto vizuri na kuwapa mwenendo mwema wa malezi ya kimaanawi.

59. Usitumie fedha zake bila ruhusa yake, hata kama itakuwa kwa ajili ya kutoa sadaka, labda kama una uhakika kwamba ataridhia.

60. Jitahidi kuwaweka watoto katika muonekano mzuri, mavazi safi n.k. Wape chakula chenye virutubisho, zingatia sana afya yao, elimu na maadili mazuri. Wafundishe Uislamu na uwasimulie visa vya mitume na maswahaba.

Ninamuomba Allah azijaze nyumba na nyoyo zetu utuvu, upendo na kuhurumiana sasa na hata milele!!!

Ungana nami katika mada ya “MKE ANAWEZA KUMSHAURI MUME BILA KUMVURUGA AKILI NA KUMUUMIZA”

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: