JINSI YA KUFLASH SIMU AIN A ZOTE



Naombeni msaada jamani wataalamu.nataka kufungua ofisi ya kutengeneza simu.je ni kitu kipi kinahitajika ili niweze kuflash simu za aina zote?je hata nikinunua box moja tu ya universal inatosha kutumia kwa aina zote za simu?asanteni.
kama mwezi umepita nahangaika na ile samsung s4 clone ya mdogo wangu ambayo inajirestart kila muda mpaka betri iishe chaji Wataalamu wa simu za android clone , nimehangaika nayo, mafundi wa mwanza chali, juzi nimeenda kariakoo fundi akaniambia iyo lete 30k nikampa ikamshinda nikaenda kwa wawili watatu chali, sasa nikaamua kutake matter in my hands, jana nimefanikiwa kuiflash na kuiroot kabisa, nikaona si vibaya kushare ugunduzi wangu huu....
Jinsi ya kuflash simu zenye MediaTek chipset
naamini clone zote zinatumia mtk pia nahisi hata za tecno nazo zina hii chipset
1. anza kwa kuandaa mazingira ya kuflash simu yako ambayo labda iko bricked, au ina tatizo lolote kama hii yangu iliyokuwa inajirestart muda wote
vitu unavyohitaji ni
a.) drivers za simu
b.) Smart Phone flash tool
c.) Mtk Droid Tools
d.) ROM / firmware ya simu yako (hakikisha ni rom sahihi kwa model ya simu yako)
2. Tuanze sasa
a.) chomeka simu yako na iache ifanye installation ya driver zote, kama zingua install driver hapo juu(kama simu yako ni mt65xx)
b.)kwa sababu simu za clone hazijulikani model maana zina imitate original, basi tutatumia MTK droid tool kujua model ya simu yetu. fungua application na uiache italeta details zote kuhusu simu
c.) tayari taarifa za simu tumezipata , kinachofuata hapo ni kudownload firmware specific kwa ajili ya simu yetu. ROM/firmware zipo hapa (ili kudownload inabidi ujisajili kwanza) pia unaweza kugoogle utapata tu. hakikisha una extract na ndani kuwe na faili MT(model ya simu yako)_Android_scatter.txt (hakikisha kuna neno scatter kwenye jina la hili file)
d.) hapo sasa kila kitu tunacho tunaweza kuanza kuflash simu yetu...
i. ichomoe simu, kisha fungua SP flash flash tools, sehemu ya scatter-loading file weka lile .txt file nililokwambia limo kwenye folder uliloextract kule juu
pia nenda options > usb mode iwe ticked pia hapohapo kwenye options angalia DA download all > Speed > force high speed inakuwa checked
ii. click download kisha iache (usichomeke simu kwanza mpaka imalize) ikimaliza chomeka simu bila betri ukisikia mlio wa simu imekuwa connected kwenye pc haraka rudisha betri bonyeza "firmware -> upgrade" kisha tulia itaanza kuflash simu
ii. kama kila kitu kimeenda sawa utaona progress kwa rangi ya njano kama kuna makosa itatokea rangi nyekundu na maelezo
ikikamilisha successiful, itaonesha kiduara cha kijani
hapo sasa unaweza chomoa simu yako na kuiwasha na utaona inaanza kama mpya vile....
ukipenda unaweza kuiroot, kubadili IMEI, kuondoa application za kichina zote kwa kutumia MTK Droid tools
TAHADHARI: SITAHUSIKA KAMA UTAHARIBU SIMU YAKO, TRY AT YOUR OWN RISK.NI KWAKUJIFUNZA TU

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: