Hatimae Rais Magufuli ataja kiwango cha pesa anacholipwa kama mshahara wa Rais Tanzania


Baada ya baadhi ya Wabunge wa vyama vya upinzani Tanzania kumtaka Rais Magufuli kuanika hadharani mshahara wake pamoja na makato ya kodi, President Magufuli ambaye ni Rais wa awamu ya tano kwenye Jamuhuri ya muungano wa Tanzania amekubali kuutaja mshahara wake.
Kama kawaida yake yeye ni shabiki wa kipindi cha TV cha Clouds 360 on CloudsTV ambacho alikipigia simu kwa suprise March 17 2016, sasa wakati anatazama kipindi hicho April 1 2016 akiwa nyumbani kwao Chato, Rais Magufuli akaona Watangazaji wakisoma magazeti na kukawa kuna habari moja kwamba Wabunge Zitto Kabwe na Tundu Lissu wanamtaka ataje kiwango cha mshahara anaolipwa kama rais wa Tanzania.
Magu
Muda mfupi baadae President aliwasiliana na Watangazaji wa Clouds360 na kusema mshahara wake ni shilingi za kitanzania MILIONI 9.5 na akasema yuko tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake na kutoa mchanganuo akimaliza mapumziko Mkoani Geita
Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: