vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiendeleza uchimbaji wa mabwawa mengine ya samaki
hili ni moja ya mabwawa ya Samaki ambalo bado linavifaranga
Hili ni moja ya Bwawa ambalo tayari Samaki wake wako tayari kuvuliwa
Vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiwavua samaki katika mabawa yao
samaki waliokwisha kuvuliwa
Mwenyekiti wa Ludewa Ash-tech Group Bw.Deogratius Sanga akionesha samaki wanaopatikana katika Mabwawa yao
vijana wa Ludewa Ash-tech group wakiendeleza uchimbaji wa mabwawa mengine ya samaki
Vijana wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe wameamua kuachana na tabia ya kucheza
mchezo wa pool nyakati za machana na kuanzisha vikundi vya uwekezaji ikiwa
pamoja na ufugaji wa Samaki,Nyuki,Uchimbaji wa visima pamoja na upandaji miti
ikiwa ni lengo la kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.John Pombe Magufuli katika kujiinua kiuchumi.
Hayo
yamesemwa leo wilayani hapa na mmoja wa vijana hao ambaye ni Mwenyekiti wa
Ludewa Ash-tech group Bw.Deogratius Sanga alisema kuwa katika kikundi hicho
kuna vijana 1o wakiwemo wakike 3 na wakiume 7 ambao awali walikuwa
wakijihusisha na michezo ya pool na kusahau miradi yao ambayo waliianzisha ikiendelea
kufa.
Bw.Sanga
alisema kuwa kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2011 lakini usajiri kamili
kimesajiriwa mwaka 2016 kikiwa na malengo ya uelimishaji kwa jamii hasa vijana
katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti,ufugaji wa Nyuki,ufugaji
wa Samaki na uchimbaji wa visima lakini katika malengo hayo yote waliweza
kufanikisha machache na kuendelea starehe za mitaani ikiwemo uchezaji pool.
Alisema kuwa
mpaka sasa Ludewa Ash-tech group wameweza kufanikisha katika ufugaji wa nyuki
kuwa na mizinga 46,wameweza kuchimba visima 54 katika makazi ya watu,wamepanda
miti ekali 12 na kuwa na mabwawa mawili ya Samaki lakini miradi hiyo yote
ilikuwa katika hali mbaya kutokana na kutokuwa na uendelezaji lakini kwa kauli
ya Mh.Rais wamepaswa kurudi katika miradi yao na kuiendeleza.
“Ludewa
Ash-tech group kama tungeendelea na utaratibu wetu wa zamani tungekuwa mbali
kimaisha lakini kutokana na kauli ya Rais wetu imetubidi kurudisha kikundi
chetu na kufanya kazi ambazo vijana wote wa Tanzania wanapaswa kutuiga kwani
tumefika katika mabwawa yetu ya Samaki tumekuta kunasamaki wakubwa mno hivyo
imetupa moyo na tumeanza kuchimba mabwawa mengine tena ili kujipatia kipato”,alisema
Bw.Sanga.
Bw.Sanga
alisema kuwa vijana wengi nchini wanahitaji msukumo wa viongozi wa juu wa
kitaifa kwani kwa kutofanya hivyo wataendelea kufanya starehe huku wazee ndio
wakiwa wazalishaji mali hivyo aliwataka vijana kutumia nguvu zao katika
kuzalisha na sio kushinda vijiweni na kucheza pool nyakati za mchana.
Aidha katibu
wa Ludewa Ash-tech group Bw.Salvius Mwanyika alisema kuwa jambo linalowakatisha
tamaa vijana kushindwa kutumia nguvu zao mashambani ni ukosefu wa mitaji kwani
wao awali waliweza kuchangishana fedha kwaajili ya kununua vifaranga wa Samaki
na mbegu za miti ambapo waliziwatika mbegu hizo za miti na baadae kuipanda
miche katika mashamba ya urithi.
Bw.Mwanyika
alisema kuwa mpaka sasa wameweza kupanda miti katika ekali 12 na kuwa na
mizinga ya Nyuki 46 hiyo yote kutokana na kila mmoja wao kujitolea na sio
ufadhiri kutoka kwa wahisani hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuliunga mkono
kundi hilo ili liweze kutoa elimu kwa vijana wengine ambao bado wako vijiweni.
Alisema kuwa
changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa eneo au Ardhi ya kufanyia miradi
yao hivyo ameiomba Serikali kuwaunga mkono katika hilo ili waweze kuzalisha
samaki wengi ambao wataweza kuwainua
kiuchumi wao na familia zao ambazo zinawategemea.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment