Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na
mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na
hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache
sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio
kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.Binadamu
ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba
binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu
anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye
kikombe na umgorogee na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo
subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari
imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi, kitu cha
kujiuliza je, mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai
yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu. Mtu
huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi
biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi biashara
yeyote tatizo nini? Atamsikia anakujibu tatizo mtaji huku akiamini kuwa
mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa makala hii hata
uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya matumizi ya fedha,
hata ukipewa milioni mia moja leo hizo pesa zitaisha utajikuta mwisho
wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama mitaji kama fedha
peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu mpaka mwisho huku
maisha yakiendelea kuwa magaumu.
Soma; Mambo 5 Yatakayokupa Hamasa Katika Safari Yako Ya mafanikio.
Ngoja
nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja nguvu
ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate fedha.
Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na mawasiliano
unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa computer na
kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza vipi kubadili
ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi tunapofeli kwa
sababu ni wavivu wa kufikiri.
|
USISUBIRI KILA KITU KUFANYIWA. |
Naendelea
kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivyokuwa na tabia za
lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta anaishi mazingira machafu ambayo
yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta binadamu
huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini mazingira haya ni machafu,
utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali, binadamu
huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini hauna ajira?
Atakujibu tatizo ni serikali.Kuna msanii mmoja wa hapa
nchini aliwahi kuimba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana
imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya
nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri
serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako
fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa
wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya
mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.
Soma; Mambo 6 Ambayo Mjasiriamali Anatakiwa Kuyafanya kila Siku.Kitu
cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi
wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata yule unayemlalamikia hakusikii
na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo
mmoja bila kusubiri mtu fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi
huu “kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari’’Mafanikio
ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo
ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa kiswahili unasema kila binadamu ni
mchungaji ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga
nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi
kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma
makala hii endapo utaulizwa swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha
uone una thamani gani mbele ya watu wengine?
Ludewa yetu na maendeleo yetu
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment