watoto wakula chakula cha mchana
Mh.Monica akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chule pamoja na watoto wa mahitaji maalumu
mwandishi Nickson Mahundi akiwa na mmoja wa watoto hao
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani wa kata ya
Ludewa katika mkoa wa Njombe kupitia chama cha mapinduzi(CCM) Bi.Monica Mchilo
ametoa mchango wake wa kilo 20 za sukari katika msimu huu wa sikuu ya Pasaka
katika kituo cha watoto wanye ulemavu wa Ngozi na wanaoishi mazingira hatarishi
ili kuwaunga mkono kwa jitihada zao za kulea watoto hao.
Akitoa
msaada huo Mh.Monic alisema kuwa watoto hao wanahitaji uangalizi mkubwa kwani
bado matondo ya kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi hayajafika wilayani
Ludewa hivyo ni vema walezi wa watoto hao kuwa makini na baadhi ya watu
wanaotembelea kituo hicho ambacho ndio cha kwanza wilayani Ludewa kuanzishwa.
Alisema kuwa
msaada huo wa sukari kilo 20 ametoa kutokana na kuguswa na huduma na uendeshaji
wa kituo hicho ambacho kinatambulika kwa jina la NICOPOLIS ACADEMY kwani
kimekuwa kikiwafundisha watoto hao tofauti na shule nyingine zote za watoto
wilayani hapa.
Aliwataka
wadau mbalimbali kuchangia kituo hicho ili kuwawezesha watoto hao kupata
chakura bora na malazi salama kwani bado kinaendeshwa na wamiliki kwa
kujichangisha michango yao hali inayowafanya wamiliki wa chule hiyo licha ya
kutoa elimu bora bali kudhohofisha familia zao kiuchumi.
“nimependa
uanzishwaji wa kituo hiki kwani nimejionea kwa macho yangu na kusikia kwa
masikio yangu elimu wanayopata watoto wadogo kama hawa ambao wanauwezo mkubwa
wa kuongea lugha ya kiingereza tofauti na shule nyingine za watoto zilizopo
hapa Ludewa Mjini,nawaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi ili
kuwaendeleza watoto hawa”,Alisema Mh.Monica.
Akishukuru kwa
msaada huo mkuu wa kituo hicho Mwalimu Augustino Mwinuka alisema kuwa Diwani
huyo ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya amekuwa mfano wa kuigwa kwa madiwani wengine
katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa kushiriki katika mambo ya kijamii.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwahudumia watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi na wale wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwapatia elimu
bora lakini kutokana na utendaji kazi mzuri wa walimu wa kituo hicho baadhi ya
wananchi wameanza kuwaleta watoto wao huku wakichangia kidogo.
Alisema licha
ya kuwa kuna baadhi ya hao wazazi walioamua kuwaleta watoto wao na kuchangia
gharama nafuu pia kituo hicho kina kabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba
wa majengo na ukosefu wa fedha za kuendeshea kituo hicho.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa amelazimika kuibomoa nyumba yake aliyokuwa akiishi na kuhama
kutafuata nyumba nyingine ya kuishi ili nyumba hiyo itumike kama madarasa ya
kusomea watoto hao ambapo amefanikiwa kugawa madarasa mawili ambayo ndio
yanayotumika kufundishia.
Alisema kuwa tayari amepata eneo linalokadiriwa kuwa hekali 7 ambazo zinafaa kwa ujenzi wa madarasa,mabweni na viwanja vya michenzo lakini changamoto iliyoko ni ukosefu wa fedha za kufanya ujenzi wa vitu hivyo hivyo anawaomba wadau mbalimbali na wafadhiri kumuunga mkono katika ujenzi wa madarasa hayo kwaajili ya watoto hao wenye mahitaji maalumu
Na habari ludewa blog
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment