Familia mseto kama hizi kupinduana hutokea sana
Unapoishi
nyumbani na ndugu yako, jamaa yako au hata mtumishi wa kike, ni vizuri
ukajitahidi kulinda ndoa yako. Kumbuka kwamba, wanaume hawajali hisia,
hujali zaidi mwili. Kama ukimwachia ndugu yako, jamaa au rafiki yako
kumzoea sana mumeo, jua tu kwamba, inawezekana unajitengenezea maumivu
makubwa sana hapo baadae.
Tafiti
zinathibitisha sana kwamba, mwanaume anapohisi kuwa mwanamke fulani
anamwonesha kwamba, yeye ni mwanaume kweli kweli, anapoonesha kwamba,
anatambua uwepo wake na mchango wake katika familia, mwanaume huanza
kumpenda, bila kujali sura au hadhi.
Kama
ndugu yako ni mjuaji wa mambo haya, anaweza kumwonesha mumeo kwamba,
anaamini kuwa ni mwanaume kwelikweli. Hii hufanyika kwa kumsifu,
kutopingana naye, kumpongeza mara kwa mara na kumwonesha kwamba anaamini
katika yeye.
Hata
wale watumishi wa ndani, wanaochukuliwa na wanaume za watu hawafanyi
hivyo kwa sababu, ati hao watumishi ni wazuri sana wa sura au wanajua
sana mapenzi, hapana.
Wanaume
huwachukua kwa sababu, wake au wapenzi wa wanaume hao wameshindwa
wajibu wao, wameshindwa kujua kwamba wanaume hutazama uhusiano kwa jicho
tofauti.
Lakini,
iwe ndugu au jamaa zenu na hata watumishi majumbani mwenu, bado na wao
ni binadamu, wana udhaifu. Kwa udhaifu wao, pamoja na udhaifu wa wanaume
au wapenzi wenu, wanaweza kuwasaliti. Kwa hiyo ni juu yenu kulinda ndoa
zenu, ili udhaifu huo usiwe chanzo kwa kuvunjika kwa matumaini na
matarajio yenu ya kujenga familia.
Kuna
mambo mawili makubwa hapa, kwanza inawezwekana mmejiachia wazi sana
kama wanawake na kusahau kuwa wanaume huvutiwa na mambo gani.
Kwa hali hiyo, mnawaacha wale walio karibu nao kuwafanyia yale wanayohitaji na kuchukua nafasi zenu.
Lakini
pili, ni udhaifu wa kibinadamu na zaidi kwa wanaume, linapokuja suala
la mwili. Kwa udhaifu huo, inabidi muwasaidie kuwalinda wasishawishiwe
kirahisi. Lakini, ndugu zenu wa kike au watumishi mnaoishi nao, inabidi
muwakague vizuri na kuacha kuwamini kupita kiasi kwa waume au wapenzi
wenu.
Ni hatari sana kwa mwanamke kwa mfano, kumwambia au kumruhusu mumewe aende sehemu za starehe na rafiki yake wa kike au na ndugu yake wa kike, ati kwa sababu anamwamini rafiki huyo au mumewe. Kumbuka, suala hapa sio kuaminika au kutoaminika, bali ukweli wa kimaumbile pia. Mwanamke, chunga ndoa yako, ilinde sana, kwani sio dhambi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment