LICHA KUSAKAMWA, WENGER ASISITIZA YUPO ARSENAL MSIMU UJAO!




WENGER-KILIO-OLDTRAFFORDHUKU akisongwa na presha kubwa ya kumaliza Msimu mwingine bila Taji la England na bila Kombe lolote, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesisitiza bado atakuwepo Emirates licha ya kusakamwa atimue.BPL-MAR20B
Baada ya kutupwa nje ya FA CUP, Kombe ambalo walilitwaa kwa Misimu Miwili mfululizo iliyopita, na pia kutolewa toka UEFA CHAMPIONZ LIGI huku wakisuasua kwenye Ligi Kuu England wakiwa Nafasi ya 3 na Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City, Wenger amekuwa akishambuliwa toka kila upande.
Lakini Wenger, ambae Msimu ujao ndio Mwaka wake wa mwisho wa Mkataba wake wa sasa wa Miaka Mitatu, amesisitiza atarejea akiwa tayari kupigana tena akiiongoza Arsenal.
Ameeleza: “Hatukustahili kupondwa. Mimi natoa nguvu zangu zote kwa Klabu ninayoipenda na kama Mashabiki watachangia mapenzi hayo ni bora. Nina ari na nina hakika nitakuwepo Msimu ujao!”
Wikiendi hii inayokuja, Arsenal wako kwao Emirates kucheza na Watford Timu ambayo ndio ilwang’oa toka FA CUP hapo hapo Emirates Wiki 2 zilizopita kwa kuwafunga 2-1.
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford              
1700 Bournemouth v Man City    
1700 Norwich v Newcastle          
1700 Stoke v Swansea               
1700 Sunderland v West Brom    
1700 West Ham v Crystal Palace  
1930 Liverpool v Tottenham                 
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton    
1800 Man United v Everton        


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: