EL CLASICO: JUMAMOSI BARCA V REAL, MBIO ZA MSN V BBC, RONALDO, SUAREZ, MESSI, NEYMAR MBIO UFUNGAJI BORA

ELCLASICO-APR1JUMAMOSI Aprili Mosi huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain, ipo Mechi kubwa ambayo Siku zote hubatizwa ‘El Clasico’, ikimaanisha ni Mechi ya kipekee ya hali ya juu kabisa, katika ya Mahasimu FC Barcelona na Real Madrid.LALIGA-STAND-MAR29
Mechi hii ni ya La Liga na inazikutanisha Barca ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi hiyo wakiongoza kwa Pointi 10 mbele ya Timu ya 3 Real huku Mechi zikibaki 8.
Timu ya Nafasi ya Pili ni Atletico Madrid ambao wako Pointi 9 nyuma ya Barca na Pointi 1 mbele ya Real.
Hii ni El Clasico ya pili Msimu huu baada ile ya kwanza ya La Liga huko Santiago Bernabeu kumalizika kwa Real 0 Barca 4.
Lakini hii ni El Clasico ya kwanza kwa Meneja wa Real, Zinedine Zidane, ambae alitwaa wadhifa baada ya kutimuliwa Rafa Bemitez Mwezi Desemba.
LALIGA-TOP-MAR29Kazi kubwa kwa Zidane ni kusaka njia ya kuwazuia Washambuliaji Mtu 3 za Barca, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, ambao wamebatizwa MSN, na ambao kati yao wamefunga Jumla ya Mabao 69 kwenye La Liga.
Lakini wenzao wa Real, Gareth Bale, Karim Benzema na Cristiano Ronaldo, wakijulikana kama BBC, wamefunga Bao 63 za La Liga huku Ronaldo ndie akitamba kuwa Mfungaji Bora wa Ligi hii akiwa na Mabao 28.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Bravo; Alves, Pique, Mascherano, Alba; Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suárez, Neymar
Real Madrid (Mfumo 4-3-3): Navas; Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo; Modric, Isco, Kroos; Benzema, Bale, Ronaldo
LA LIGA
Jumapili Machi 20
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Aprili 1
2130 Rayo Vallecano v Getafe CF
Jumamosi Aprili 2
1700 Atletico de Madrid v Real Betis
1915 Las Palmas v   Valencia C.F
2130 FC Barcelona v Real Madrid CF
2305 Celta de Vigo v Deportivo La Coruna
Jumapili Aprili 3
1200 Athletic de Bilbao v Granada CF
1600 Malaga CF v RCD Espanyol
1815 SD Eibar v Villarreal CF
2030 Sevilla FC v Real Sociedad
Jumatatu Aprili 4
2030 Levante v Sporting Gijon



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: