KILELE CHA WIKI YA MAJI WILAYANI LUDEWA CHAADHIMISHWA KWA KUPANDA MITI KATIKA VYANZO VYA MAJI




Miti inayohifadhi maji ikiwa imepandwa
 Miti inayohifadhi maji ikiwa imepandwa

 kaimu meneja wa mamlaka ya maji Ludewa Bw.Gregory Mwinuka akipanda miti katika chanzo kimojawapo cha maji Mapetu siku ya kilele cha wiki ya maji
Bw.Esau Haule ni mmoja wa wananchi waliokubali kuachia maeneo yao ili kuhifadhi vyanzo vya maji

 kazi ya upandji miti ikiwa inarndelea








Kilele cha wiki ya maji wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimeadhimishwa kwa upandaji miti katika vyanzo vya maji katika maeneo ya Mapetu huku wananchi wakikubali kuachia maeneo yao ambayo yako katika vyanzo hivyo awali yalitumika kama mashamba yao ili kuweza kupata maji kwa wingi katika uhifadhi wa Vyanzo hivyo.

Akiongea na waandishi wa habari mmoja wa wananchi wenye maeneo katika vyanzo hivyo ambaye alishiriki katika upataji wa miti inayoweza kuhifadhi maji Bw.Esau Haule alisema kuwa awali vyanzo hivyo vilitumika kama mashamba ya vinyungu na kuweza kuwasaidia wakulima hao katika kipato lakini walipotakiwa kuayaachia maeneo hayo walifanya hivyo bila kukaidi.

Bw.Haule alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa hakuna asiyejua umuhimi wa maji katika matumizi ya binadamu hivyo tamko la Serikali la kupisha eneo hilo la Mapetu ili kuweza kuhifadhi chanzo hicho cha maji hakuna mwananchi ambaye alipinga na hivyo yeye ambaye alikuwa na eneo kubwa katika chanzo hicho amelazimika kushiriki kikamilifu kupanda miti ambayo itaendeleza utunzaji wa chanzo hicho.

Alisema kuwa kuna baadhi ya wakulima bado hawanaelimu ya kutosha kuhisiana na kuhifadhi vyanzo vya maji hivyo Serikali inapaswa kutoa elimu mara kwa mara kwani asilimia kubwa ya wakulima wa wilaya ya Ludewa bado wanatabia ya kulima katika vyanzo vya maji hasa nyakati za kiangazi.

Bw.Haule alisema changamoto kubwa inayovikabili vyanzo vya maji ni pamoja na uchomaji moto kwa wawindaji na wachomaji mkaa ambapo moto hutoroka na kuteketeza magugu yanayosaidia utunzaji wa vyanzo hivyo hali hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara hasa baada ya msimu wa mvua kuisha hivyo Serikali inatakiwa kuwachukulia hatua za kisheria wenye tabia hizo.

“Nimeshiriki katika zoezi hili la upandaji miti siku ya kilele cha maji ili kuwaonesha wananchi wenzangu umuhimu wa jambo hili kwani bila kufanya hivi wananchi wangeweza kuona bado ninakinyogo na kutoa eneo langu ili litumike kama eneo la kuhifadhi chanzo hiki cha maji,hivyo nawaomba wengine kuiga mafano huu”,alisema Bw.Haule.

Naye kaimu meneja wa mamlaka ya maji Ludewa Mjini Bw.Gregory Mwinuka alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhifadhi vyanzo vyote vya maji wilayani Ludewa ili kuweza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi isiyo na mashaka msimu mzima wa mwaka.

Bw.Mwinuka alisema kuwa ifikie wakati wananchi watii sheria bila shuruti kwa kuacha kuvamia vyanzo vya maji na kulima mazao ya chakula nay ale ya kibiashara kwani kwa kuvitunza vyanzo hivyo kero ya uhaba wa maji itatoweka na kuwafanya wananchi wakifanya shughuri nyingine za kimaendeleo nadala ya kutafuta maji.

Mwisho.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: