Shomari Kapombe ameendelea kufunga ndani ya kikosi cha Azam FC baada kutupia tena mbao mbili kambani kwenye mchezo war obo fainali ya kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Azam kuibuka na ushindi wa bao 3-1 hatimaye vigogo hao wa Temeke kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kapombe alianza kuifungia Azam FC dakika ya 9 kipindi cha kwanza baada ya mpira kuzangaa kwenye eneo la hatari kisha Kapombe akageuka na kuachia shuti kali lililoja moja kwa moja wavuni
Jeremia Juma alipiga bao la kusawazisha kwa upande wa Tanzania Prisons dakika ya 31 kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo kwenda mapumziko huku timu hizo zikiwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kipindi cha pili Azam ilianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumpumzisha Waziri Salum na nafasi yake ikachukuliwa na Frank Domayo dakika ya 48 kipindi cha pili.
Dakika mbili baadaye baada ya mabadiliko hayo, Shomari Kapombe akaiweka tena mbele Azam FC kwa kupachika bao la pili kwa upande wa Azam.
Dakika ya 86 Hamisi Mcha akaipatia Azam bao la tatu na kuihakikishia timu hiyo kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA.
- Kwa mujibu wa takwimu za shirikisho la soka Tanzania (TFF) Kampombe anamagoli 8 huku akifanikiwa kutupia bao mbili wavuni leo kwenye mchezo wa FA.
- Azam imekuwa ikisuambuana na Tanzania Prisons kwenye mechi zake za ligi, kwenye mechi tatu za ligi zilizopita Azam imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare mara mbili. 24/06/2016 Azam ilitoka sare ya bila kufungana na Prisons, 12/09/2015 Azam lishinda kwa magoli 2-1 dhidi ya Prisons wakati 21/02/2015 timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment