IJUE Pasaka ya Kikristo






Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulibiwa kwake. Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika Ukristo.





Jina la Pasaka






Jina la "Pasaka" limetokana na sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi linaloitwa "פסח" (tamka: pasakh) kwa lugha ya Kiebrania. Kwa Kiswahili majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani. Asili yake ni ya kwamba kusulibiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamo mwaka 30 BK. Wakristo wa kwanza ambao wote walikuwa Wayahudi walisheherekea sikukuu ya kiyahudi pamoja na kumbukumbu kwa ufufuo wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti.





Tarehe ya Pasaka



Tarehe ya Pasaka inafuata mwezi kwa hiyo sikukuu hiyo haina tarehe imara katika kalenda ya kawaida. Inapatikana katika Machi au Aprili. Mtaguso au Sinodi Kuu ya Nikea mwaka 325 BK iliamua ya kwamba Pasaka itasheherekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya Machi 21 (tarehe ya sikusare machipuo ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku hivyo mwanzo wa majira ya kuchipua katika kaskazini ya dunia). Kwa sababu mwezi mpevu baada ya Machi 21 inaweza kutokea kati ya Machi 22 na Aprili 19 tarehe ya Pasaka ambayo ni Jumapili inayofuata hutokea kati ya Machi 22 na Aprili 25.

Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika hivyo pia tarehe mbili za Pasaka. Makanisa ya magharibi yaani Wakatoliki na Waprotestant hufuata Kalenda ya Gregori (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia yaani Kalenda ya Juliasi.


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: