Rais
Mteule wa Zanzibar Dk. Mohammed Shein aliyeshinda uchaguzi wa marudio
uliofanyika Jumapili iliyopita, ataapishwa leo katika Uwanja wa Amaan
mjini Unguja.
Katika
tukio hilo la kihistoria, viongozi mbalimbali wa kitaifa wanatarajiwa
kuhudhuria wakati rais huyo wa awamu ya saba akiapa kuanza awamu yake ya
pili ya uongozi wa taifa hilo lenye visiwa viwili vya Unguja na Pemba.
Rais
Shein alishinda uchaguzi huo wa marudio, kufuatia Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kufuta matokeo ya
uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kwa kile alichodai kuwepo kwa
dosari kutoka kwa baadhi ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Hata hivyo, baadhi ya vyama vya siasa vikiwemo Cuf na ACT-Wazalendo vilisusia uchaguzi huoLudewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment