UTANI WA MAKABILA

Kwa sisi wengine tuliozaliwa mijini tuna mchanganyiko sana wa makabila. Na mara nyingi makabila hayo hayana uhusiano kabisa wala hayatoki kwenye mkoa mmoja. Kuzaliwa mjini kumetusaidia sana kujua tabia za makabila mbali mbali. Haya ni maoni yangu yanayotokana na uzowefu wangu.

1. Waluguru = Wanapenda wageni, wafanyabiashara Sokoni, waumini wazuri, mashabiki wakubwa wa mpira wa Miguu

2. Wangindo na wandengereko = Wanaamini dini za asili, wanashirikiana, wanathamini sana wajomba na mama zao

3 Wajaluo = Wajivuni, wanapenda maendeleo, washika mila, wanapenda burudani, wanapenda uzungu

4 Wamanda/wapogoro/wambunga.= Hawana choyo, waburudishaji, wanafamilia, waumini wazuri,wanashikamana.

5. Wanyiha/wasafwa/wapangwa= Washika dini, hawapendi kuingiliana na watu,wanashikamana

6. Wamwera/Wayao = Mahiri kwenye matumizi ya lugha, wanasanaa wa mahusiano, wanaheshimu sana wajomba na mama zao.

7. Wamanyema = Wapenda majadiliano, waumini wazuri,manju, watembezi,wanashikamana

8. Wapare = Washika kanuni, watunza mali, wapenda mijadala, waumini wazuri, wahafidhina.

9. Wafipa = Wahafidhina, washika dini, wanashikamana, wapole, watamaduni

10. Wavidunda/Wasagara/Wasaki/wakaguru/wakutu = wanashikamana, wanafamilia,wanautamaduni

11. Wagogo = Waburudishaji, wanafamilia,waumini wazuri, wapenda sanaa, wanashikamana

12. Wakurya = Wana misimamo, wakweli,wanautamaduni,washindani,wapenda maendeleo

13. Wachagga = Wachakarikaji,waumini wazuri, wapenda maendeleo,wanashikamana

14. Wangoni = Wajivuni, waumini wazuri, watembezi,jasiri, si wasiri

15. Wakwere = Wapole, waumini wazuri, wanautamaduni,wanashikamana,wasiri,

16.Wahaya = Wajivuni, wanapenda elimu, wanapenda maendeleo,waumini wazuri, wanashikamana

17. Wanyamwezi = wapole, waumini wazuri, wanautamaduni,manju,wahafidhina,watembezi,hawashikamani

18. Wapulu = wakimya,wanautamaduni, wajadi, si watembezi,hawajitambulishi kwa jamii (Exposure)

20.Wazanaki = wanatafakuri, Manju, wahafidhina, waumini wazuri, si watembezi, wanashikamana


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: