KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU AKIMPOKEA MWENYEKITI WA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI AMBAYE NI MKUU WA MKOA DKT REHEMA NCHIMBI AKISALIMIANA NA MBUNGE WA JIMBO LA MAKAMBAKO DEO SANGA
AWALI KABLA MKUU WA MKOA ALIPOKUWA HAJAWASILI UKUMBI WA KIKAO KATIBU TAWALA AKISUBILIA
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI SKIHUTUBIA WAJUMBE WA KAMATI HIYO WAKATI WA UFUNGUZI WA KIKAO HICHOMKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO AKIWA NA HANANA MFIKWA AMBAYE NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO
WATUMISHI KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WANAWEKANA SAWA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA WA KATIKATI NA ANAYETAZAMA SIMU NI MBUNGE WA LUDEWA DEO NGARAWA NA WA KUSHOTO NI EDWARD KAZIMOTO AMBAYE AMEMUWAKILISHA ASKOFU WA KANISA LA ANGLIKANA DIOSISI YA KUSINI.
WATAALAMU MBALIMBALI WA MKOA
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE
Mkuu Wa Mkoa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Ameagiza Halmashauri Zote Za Mkoa Huo Kuhakikisha Zinamaliza Tatizo La Madawati Katika Shule Zilizopo Kwenye Halmashauri Hizo Pamoja Na Kujenga Maabara Ifikapo June Mwaka Huu Ili Kuboresha Kiwango Cha Elimu Kwa Wanafunzi.
Akizungumza Na Kamati Ya Ushauri Mkoa ,Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amesema Halmashauri Hizo Zinatakiwa Kujadili Namna Zitakavyoendesha Shule Zote Za Serikali Zilizopo Maeneo Yao Ikiwemo Kutengeneza Madawati Kuanzia Shule Za Chekechea Hadi Kidato Cha Nne Pamoja Na Utoaji Tuzo Kwa Walimu Wanaofaurisha Vizuri.
Katika Hatua Nyingine Dkt Nchimbi Amekanusha Kuziaguza Halmashauri Kuanzisha Mfumo Wa Wanafunzi Kushonewa Sare Za Shule Kwa Lazima Na Kusema Kuwa Kikao Cha Ushauri Cha Mkoa Kilikubaliana Kuanza Zoezi La Kushona Sare Hizo Kwa Hiari Na Siyo Kulazimisha Wazazi Kuwashonea Watoto Wao Sare Hizo.
Wakichangia Hoja Ya Kushuka Kwa Ufauru Wajumbe Wa Kamati Ya Ushauri Mkoa Wa Njombe Akiwemo Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Wanging'ombe Antony Mahwata Na Baadhi Ya Wabunge Wameshauri Ukaguzi Kufanyika Mara Kwa Mare Kwenye Shule Hizo Pamoja Na Kuboresha Mazingira Ya Kufundishia.
Wamesema Elimu Bure Shuleni Imewakatisha Nia Walimu Ya Kufundisha Wanafunzi Kutokana Na Kukosekana Kwa Fedha Za Kuendeshea Shule Hizo Ambapo Wazazi Wakiombwa Kupeleka Baadhi Ya Michango Wamekuwa Wakigoma Kuchangia Kutokana Na Tangazo La Rais Kwamba Elimu Bure Huku Fedha Za Kuendeshea Zikiwa Hazijapelekwa.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment