DC MAKONDA ATOA SIKU 20 WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MITAA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM WAPEWE RAMANI ZA MITAA YAO





Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza na Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo kwenye mkutano uliofanyika Dar es Salaam leo kuhusu jinsi ya kutatua na kukomesha kero za ardhi
Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Makonda (hayupo pichani)

Na Dotto Mwaibale

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ametoa siku 20 kwa Wenyeviti wote wa Serikali za Mitaa Manispaa hiyo kuwa na ramani ya mitaa ili kuyatambua maeneo ya wazi.Makonda amewataka watendaji wa Manispaa hiyo kwenda na kasi ya serikali ya kuwatendea haki wananchi katika kumaliza migogoro ya ardhi.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana na Wenyeviti zaidi ya 100 wa Serikali za Mitaa ya9 Manispaa ya Kinondoni ,Makonda alisema baadhi ya watendaji wanatanguliza maslahi mbele kuliko mahitaji ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema migogoro ya ardhi ni kero kila sehemu misibani, harusini na kwenye mazishi suala kubwa ni la ardhi na kuongeza kuwa mabaraza ya ardhi ya Kata hayana uhalali wa kuamua kesi hizo kwa kuwa baadhi yao hata uelewa wa masuala hayo hawana na yamekuwa yakiongeza matatizo.

"Leo tumekutana hapa kwa sababu ya migogoro ya ardhi na kuanzia sasa ndani ya Wilaya ya Kinondoni nataka kurudisha heshima ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa nawaagiza kuanzia sasa mtu yeyote kutoka Wizarani,Manispaa au hata mwekezaji lazima apitie kwanza kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa,"alisema.

Alisema watendaji wengi Manispaa ndio chanzo cha migogoro ya ardhi kwa kutotimiza wajibu wao na wameshindwa kuonyesha dira ya kuwasaidia wananchi."Kibaya zaidi ili kujitengenezea mazingira ya ulaji wenyeviti hawashirikishwi katika hatua za awali wanahusika zaidi pale kunapotokea mgogoro,"alisema.

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: