CCM MKOA WA NJOMBE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUYAPOKEA MABADILIKO YALIOPO



 KATIBU CCM MKOA WA NJOMBE HOSEA MPAGIKE  MARA BAADA YA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Halmashauri Kuu  Ya  CCM Mkoa Wa Njombe  Imewataka Watumishi Wa Umma  Kuyapokea Mabadiliko Ya Utendaji Kazi  Na  Kuacha Kufanya Kazi Kwa Mazoea  Badala Yake Wafanye Kazi Kwa Uadilifu,Uwajibikaji ,Uhodari Wa Kazi  Na Bidii  Na Ufaanisi  Kwa Lengo La Kuharakisha Maendeleo Kwa Faida Ya Watanzania Wote.

Rai Hiyo Imetolewa Na  Katibu Wa CCM  Mkoa Wa Njombe  Hosea Mpagike Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Kikao  Cha  Ndani Cha Halmashauri Kuu   Kilichodhamilia Kujadili Mambo Mbalimbali Ya Maendeleo  Ya Chama  Ikiwemo  Kutoa  Tathmini Ya Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Mwaka Jana.

Aidha Mpagike Amesema  Miongoni Mwa Mambo Yaliopewa Kipaumbele Kwenye Kikao Hicho Ni Pamoja Na  Watumishi Kufanya Kazi Kwa Uadilifu,Kujituma  Na Uwajibikaji Kwa Manufaa Ya  Watanzania Wote  Ili Kuendana Na Kasi Ya Uongozi Wa Awamu Ya Tano    Huku Katika Uchaguzi Huo Akisema  Chama Cha Mapinduzi Kilishinda  Kata 90 Dhidi Ya Wapinzani Wake Ambao Wameshinda Kata 17.
Mpagike  Amesema Halmashauri  Hiyo Pia  Imepongeza Utendaji  Kazi  Na Utekelezaji Wa Ilani  Wa Chama Hicho Wa Rais  Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri  Kwa Siku 100 Tangu Kuchaguliwa  Ambapo Amefanikiwa  Kupambana Na Maovu Nchini Ikiwemo Kukemea Vitendo Vya Rushwa,Ujangile,Madawa Ya Kulevya ,Uzemba Na Wizi Wa Mali Za Umma.

Amesema  Swala Lingine  Lililotajwa Na Halmashauri Hiyo  Ni Pamoja Na  Dr Magufuli  Kuanza Kutekeleza   Uboreshaji Elimu Kwa Kuondoa Ada Kwa Shule Za Msingi Na Sekondari Kuanzia Kidato Cha Kwanza  Hadi  Cha Nne Jambo Ambalo Limetajwa Kuwanufaisha Wazazi Waliokuwa Hawana Uwezo Wa Kupeleka Watoto Shule.

Kuhusu Miradi  Ya Serikali Iliyoshindwa Kukamilika  Kwa Kipindi Kilichopita  Halmashauri Hiyo  Imeagiza  Kupewa Kipaumbele  Cha Kukamilisha Kabla Ya Kuanza Miradi Mipya  Kupitia Bajeti Za Serikali Zinazotengwa Ambapo Amesema Kuna Majengo Ya Shule,Zahanati  Ambayo Nguvu Ya Wananchi Ilitumika Lakini Haikukamilika  Ili Ku0koa Majengo Hayo Yasiharibike.

Kikao Hicho Cha Halmashauri Kuu  CCM Mkoa Njombe  Kimefanyika  Februari 13 Katika Ofisi Ya Chama Cha  Mapinduzi   Kikiwa Na Agenda Kuu Mbili  Ikiwemo Kufanya Tathmini Ya Uchaguzi Mkuu  Wa  Rais ,Wabunge Na Madiwani Wa Mwaka 2015 Na Taarifa Ya Kazi   Za   Chama .

Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: