Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ameungana na kauli ya wanazuoni kumuomba
Rais John Magufuli kuamrisha mamlaka husika kumkamata mmiliki wa kampuni
ya IPTL/PAP yenye mitambo ya kufua umeme iliyozua sakata la ESCROW,
Harbinder Sing Sethi.
Uongozi
wa Jumuiya ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA) hivi
karibuni walimtaka Rais Magufuli kufanikisha utekelezaji wa azimio namba
moja la Bunge kufuatia sakata la Escrow.
Azimio
namba moja la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu hatua za
kuwachukuliwa dhidi ya Sethi ambaye kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya
PAC iliyokuwa chini ya uenyekitiwa wa Zitto Kabwe alisababishia taifa
hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 320, ni kuchukuliwa hatua kwa
kufanya jinai kwa kusababisha upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 320
za umma.
“Tunashangaa
mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW
hayajatekelezwa na badala yake wanaishia kuwatoa kafala akina William
Ngeleja na Anna Tibaijuka. Hii haitakiwi kuiacha hivi hivi. Lazima sisi
kama vijana wasomi tusimame kulitetea taifa letu na rasilimali zake,”
Katibu wa JUWARA, Mahmubu Salibaba aliliambia Jamvi la Habari.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment