Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na
aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya CCM,
Stephen Wassira kupinga ushindi wa Esther Bulaya (Chadema).
Wassira
alipinga vikali matokeo ya uchaguzi huo akidai kuwa uligubikwa na
udanganyifu na hujuma dhidi yake ikiwa ni pamoja na kutofautiana kwa
idadi ya wapiga kura kwenye kituo na jumla ya kura zilizoonekana kwenye
fomu za matokeo. Wassira aliiomba mahakama kubatilisha ushindi wa
Bulaya.
Bulaya
alihamia Chadema akitokea CCM na kupewa nafasi ya kugombea ubunge
katika uchaguzi mkuu uliopita na hatimaye kumshinda mwanasiasa huyo
mkongwe aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mingi na waziri wa
serikali ya awamu ya nne.
Kupitia Facebook, Esther Bulaya ameandika kuhusu hukumu ya kesi hiyo:
“
Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na
wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu
wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda
Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma
tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho.Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment