Mwamuzi wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana aliyechezesha mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi watakaoendelea kuchezesha mashindano ya Mapinduzi Cup kufuatia kulikataa bao la Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumapili January 3, 2015.
Mwamuzi huyo alilikataa bao halali lililofungwa na Kichuya wa Mtibwa Sugar kipindi cha pili cha mchezo huo ambalo lingeipa ushindi timu ya Mtibwa Sugar kwenye mcheo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kukataliwa kwa bao hilo kulizua tafrani kati ya waamuzi waliochezesha mchezo huo dhidi ya wachezaji wa Mtibwa na bechi zima la ufundi hali iliyolazimu jeshi la polisi kuwatoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Katibu wa kamati ya ZFA Hashim Salum Hashim amemwandikia barua ya kumwondoa kwenye mashindano ya Mapinduzi mwamuzi huyo kutokana na kutokuwa makini kwenye mchezo kati ya Azam FC vs Mtibwa Sugar.
Hapa chini kuna barua kutoka kwa katibu wa ZFA ya kumwondoa kwenye mashindano mwamuzi Dalila Jaffar Mtwana.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment