Khadija Mngwai, Dar es Salaam
YANGA imeondoka jana saa 4:00 asubuhi kwenda Zanzibar tayari kwa Kombe la Mapinduzi. Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema kwa kikosi walichonacho ni lazima watwae ubingwa.
Kesho Jumapili saa 10:30 jioni kwenye Uwanja wa Amaan, Yanga itacheza na Mafunzo katika mchezo wa Kundi B la michuano hiyo. Timu nyingine za Kundi B ni Azam FC na Mtibwa Sugar.
Kikosi cha Yanga kiliwasili salama jana mchana Zanzibar na leo asubuhi kilitarajiwa kufanya mazoezi ili kujiweka sawa na mchezo huo wa kesho.
Mwambusi aliliambia Championi Jumamosi kwamba, kikosi cha Yanga kwa sasa kimeimarika, hivyo wanakwenda kwenye Kombe la Mapinduzi kwa ajili ya kujiweka sawa.
“Kwa kikosi tulichonacho, hakuna shaka tunatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, hata Ligi Kuu Bara kwani tukirudi katika ligi tutakuwa vizuri zaidi kwani michuano hii itakuwa maandalizi kwetu.
“Tulikuwa hatuhitaji kushiriki michuano hii lakini kutokana na uwepo wa timu kutoka nje ya nchi ndiyo maana tumeshiriki, unajua kwa kikosi chetu cha sasa hata ligi ya bara tutatetea ubingwa bila tatizo.
“Kikosini kuna ushindani wa hali ya juu kati ya wachezaji, hilo ndilo jambo linalotufanya tujivunie timu yetu,” alisema Mwambusi ambaye ni kocha wa zamani wa Mbeya City.
Kutoka nje ya nchi, timu inayoshiriki Kombe la Mapinduzi ni URA ya Uganda ambayo ipo Kundi A sambamba na Simba, Jamhuri na JKU za Zanzibar
Ludewa yetu na maendeleo yetu
About Rafiki Fm Ludewa
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment