Mgambo wa Manispaa ya Morogoro wakiwakamata kwa nguvu baadhi ya Wananchi waliokaidi zoezi la kuondolewa kwa mama ntilie katikati ya Mji
Mgambo
wa Manispaa ya Morogoro wakishirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na
JWTZ wametumia nguvu kuwaondoa wafanyabiashara wa vyakula na matunda
wanaofanya biashara hiyo pembezoni mwa barabara zikiwa ni jitihada za
kutokomeza kipindupindu.
Operesheni
hiyo imekuja kufuatia mkoa wa Morogoro kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa
wa kipindupindu kati ya mikoa 10 inayokabiliwa na ugonjwa huo.
Baadhi ya
wafanyabiashara na mashuhuda wa operesheni hiyo wameeleza kusikitishwa
na zoezi lililofanywa na mgambo hao kwa wamewafanyia vitendo vya
udhalilishaji kwa kuwapiga bila huruma na kwamba wangetumia utaratibu
mwingie bila kuwabughudhi wafanyabiashara.
Wakizungumzia
operesheni hiyo afisa afya manispaa ya Morogoro Bw. Gabriel Malisa na
afisa tarafa Morogoro Bw. Pakapakara Mulenge wamesema operesheni hiyo
inalenga kutokomeza ueneaji wa ugonjwa wa kipindupindu na kwamba zoezi
hilo ni endelevu hadi ugonjwa huo utakapoisha.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment