Shilole amesema kuwa, haoni sababu ya kuendelea na Nuh kwa kuwa anahisi anambana tu na wala haoni faida kubwa ya kuwa naye.
Kufuatia maneno hayo, Nuh ameona isiwe kesi, amekubali yaishe lakini taarifa iliyotua kwenye ukurasa huu ni kwamba, jamaa anahaha kufuta tatuu aliyojichora mwilini mwake yenye jina la Shilole.
“Kimsingi ile tatuu ya Shilole inamtesa sana Nuh,” alisema rafiki wa msanii huyo.
Nuh anasemaje? Msikie: “Ni kweli ila hii tatuu nitaifuta nitakapompata wa kuziba pengo la Shilole.”
-GPL
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment