Nyimbo 20 za Bongofleva zilizofanya vizuri mwaka 2015

Imeandaliwa na; Steven Mwakyusa,Tumsifu Kaoza na Moringe Jonasy
Hizi ndizo nyimbo zilizofanya vizuri zaidi katika bongo flava kwa mwaka 2015
1. Nivumilie-Barakah da Prince & Ruby

2. Subira-Kassim Mganga & Christian Bella

3. Sophia-Ben Paul 

4.Nashindwa- Christian Bella 

5. No body but me-Vanessa Mdee &Kcee

6. Chekecha Cheketua-Alikiba 

7. Na yule-Ruby

8. Game-Navy Kenzo ft Vanessa Mdee

9. Nana-Diamond & Flavour

10. Shauri zao-Belle 9

11. Nikuite nani-Jux

12. Suna-Barnaba

13. Nitazoea-Mo music

14. Nusu nusu-Joh Makini

15. For u-Q chilla

16. Shikorobo-Shetta

17. Viva Roma- ROMA

18. Safari-Nick wa pili, G nako, Joh Makini & Vanessa Mdee

19. Siri-Barnaba & Vannesa Mdee

20. Aiyola-Harmonize

Hawa wameonekana kufanya  vizuri kwa mwaka unaoenda kuisha, ukiangalia kwa makini katika hii list utagundua kwamba kuna aina ya muziki ambayo inashika chart kwa sasa..na si nyingine bali ni Afro-pop!!
Ukimwangalia Shetta kabadilika kwa kiasi kikubwa, Q chilla naye alionesha mabadiliko makubwa katika ngoma ya For u, huku naye Jaffarai akijaribu kutoka katika stail yake ya zamani katika wimbo aliomshirikisha Kassim "Wakati"...ni wengine wamejaribu kuendana na wakati uliopo, pengine bahati haikuwa kwao!!
Ukiangalia nafasi ya Hip hop na RnB bado ni finyu, huu unaonekana kuwa muziki ambao unapoteza mvuto kila kukicha...wasanii wengi wameshindwa kutamba licha ya kutoa nyimbo..katika hilo kundi wamo akina Young D, Jos Mtambo, N2N pia wasanii wa Tamaduni music!!
Wapo wasanii waliofanya vizuri mwaka uliopita lakini mwaka huu wameshindwa kufurukuta, hawa ni pamoja na Recho, Mwasiti, Tumbulo, Rich Mavoko, Ommy Dimpoz, MwanaFa na Ay, Madee, D knob pia Dayna Nyange kwa kutaja kwa uchache!!
Nyota imeonekana kung'aa sana kwa Vanesa Mdee, Ruby pamoja na Christian Bella...hawa wameweza kutengeneza hits zao...na pia kufanya vizuri pale waliposhirikishwa!!
Mwisho niwapongeze wasanii wote walioweza kutengeneza nyimbo nzuri na kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki, muziki wetu unakua japo bado kuna zile kauli kwamba muziki ulikuwa zamani!! Leo si ajabu kuona nyimbo zetu zikichezwa katika radio stations na Tvs za mataifa mbalimbali! 
Bado naamini tunaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa na kuitangaza vyema nchi yetu!!

Muhimu: Orodha hii imetumia maoni binafsi ya waandishi na michango mbalimbali kutoka mitandao ya kijamii.


Happy New Year 2016!!



Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: