Sarakasi za kubadilishwa na kusimama kwa ratiba ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara imesababisha wadau wa soka nchini kuchachamaa na kuinyooshea vidole bodi ya ligi (TPBL) pamoja na shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kuiruhusu timu ya Azam FC kwenda Zambia kushiriki mashindano ambayo si rasmi na hayatambuliwi na chama chochote cha mpira wa miguu huku wakisababisha viporo kwenye ligi.
Kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameiuka na kufunguka kwamba kama kuna timu ambazo zinapagwa kuwa mabingwa basi zifahamike na zitangazwe mapema kuwa msimu huu ubingwa ni wa timu fulani na msimu ujao itachua timu ulani.
“Kuna vitu vingi sana vinafanyika vinawabeba watu fulani na kuwaumiza watu fulani, haiwezekani hii ligi kila siku inasimama pasipokuwa na sababu”, amesema Julio.
“Hakuna sababu ya kusimamisha mechi za ligi kwasababu mtu fulani anakwenda kufanya mazoezi mazoezi ambayo hayapo kwenye ratiba. Ni jakambo ambalo kwa kweli linatuumiza lakini tunakaa kimya kwa bahati mbaya tukisema tunaonekana tunawapiga watu fulani”.
“Kama ni favor basi iwe ni kwa wote au kama kuna watu wanatakiwa kupewa ubingwa basi waseme tu Yanga wachukue mwaka huu mwaka unaofuata wachukue Azam ili wawakilishe nchi”.
Jumatatu ya wiki hii Azam FC iliondoka kuelekea Zambia ambako imealikwa kushiriki michuano ya kirafiki nchini humo michuano ambayo si rasmi. Jana Azam ilianza kwa sare michuano hiyo kwa kufungana goli 1-1 na timu ya Zesco United.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment