Wazazi na walezi
wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwani
shule zimefungua lakini idadi ya wanafunzi hasa wale wa kuanza kidato cha
kwanza ni hafifu hali ambayo inawapa mazingira magumu ya walimu kuanza
kuwafundisha wanafunzi ambao wameripoti katika shule mbalimbali wilayani hapa. Hayo yamesemwa na
Afisa elimu sekondari wilayani hapa mkoani Njombe Bw,Matenus Ndumbalo wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni juu ya kasi ya
wanafunzi wa kidato cha kwanza kulipoti na kuanza masomo rasmi ndipo aliposema
kuwa kasi ya wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao mashuleni wilayani Ludewa
ni ndogo sana tofauti na miaka mingine. Afisa elimu huyo
amesema kuwa wazazi watambue kuwa walimu wanaendelea na kazi yao ya kuwajibika
kuwafundisha wanafunzi bila kujali kuna wanafunzi hawajafika huku akisema
mtihani ukitungwa hauchagui mwanafunzi aliyewahi kuanza masomo bali ni mtihani
ambao utawahusu wanafunzi wote kwa kufuata utaratibu. Hata hivyo
Ndumbalo ameongeza kuwa amejaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya shule
wilayani hapa ili kujua mwitikio wa wazazi juu ya kuawapeleka wanafunzi wa
kidato cha kwanza majibu yake ameambiwa kasi ni ndogo saana na sababu
haieleweki hivyo afisa elimu amewaomba wazazi kutekeleza majukumu yao bila
shukuruti. Katika hatua
nyingine redio best fm imemuomba afisa elimu huyo afike katika kituo cha
matangazo BEST FM ili atoe ufafanuzi kwa wananchi kuhusu suala la elimu siku ya
ju8matatu january 18 mwaka huu kwenye kipindi cha Nuru ya Asubuhi kuanzia saa
mbili kamili Asubuhi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment