Wananchi wa kitongoji cha Luvungo katika kijiji mavala
kata ya Milo wilayani Ludewa mkoani Njombe watarajie kutatuliwa changamoto ya
kituo cha Afya na barabara ya kutoka Luvungo hadi kufika Isaula
Hayo yamesemwa na Diwani wa kata ya Milo katika jimbo la
Ludewa Mh,Elisha Hule kupitia Chama cha mapinduzi ccm mapema hii leo wakati
akihojiwa na kituo hiki cha redio Best fm juu ya nini mpango mkakati wake wa
kuongeza kiwango cha maendeleo katika vijiji vyote vya kata ya milo.
Mh,Elisha amesema kuwa jambo la kwanza kabisa la
kulifanya na linatarajiwa kukamilika mwezi Decembe 2016 ni kutatua changamoto
ya zahanati na miundombinu hasa barabara ya kutoka katika kitongoji cha Luvungo
ili ifike Isaula.
Hata hivyo amesema tayari suala la changamoto ya barabara
ya kutoka kigasi kulekea milo tayari inafanyiwa marekebisho na yeye kama Diwani
wa kata hiyo tayari amesha changia kiasi cha shilingi laki tano katika
kuhakikisha barabara hiyo inakaa mkao wa kuitwa barabara.
Diwani huyo ameongeza kuwa kuna barabara ya Mholo hadi
Milo lazima ifanyiwe marekebisho mapema pamoja na kuikarabati maabara ya hospitali
ya milo huku akumshukuru Bw,Matiasi Luoga kwa kujituma katika kuwasaidia
wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment