Arsena ikiwa na wachezaji 10 imeshindwa kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Diego Costa kufunga goli na kuipa ushindi Chelsea kwenye dimba la Emirates.
Beki wa kutumainiwa wa The Gunners Per Mertesacker alizawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg baada ya kumwangusha striker wa Chelsea Diego Coata.
Costa alifunga goli dakika tano baadaye baada ya Mertesacker kutolewa kwa kadi nyekundu. Krosi iliyopigwa na Branislav Ivanovic ilimkuta Costa ambaye ailiukwamisha mpira wavuni na kuifanya Chelsea kufikisha mechi tisa za ligi bila kupoteza mbele ya Arsenal.
Ushindi ungeifanya Arsenal kurejea kileleni mwa ligi lakini ushindi wa Chelsea unaifanya Arsenal kushuka hadi nafasi ya tatu wakiiacha Leicester City ikiongoza ligi kwa pointi tatu mbele ya Manchester City.
Takwimu ambazo unatakiwa kuzifahamu
- Arsenal sasa imefikisha mechi jumla ya saa tisa na dakika 32 (9:32) bila kufunga goli kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea.
- Chelsea haijapoteza mechi hata moja ya ligi kati ya mechi tisa dhidi ya Arsenal, imeshinda mechi sita na kutoka sare mara tatu.
- Costa amefunga magoli sita kwenye mechi sita chini ya Guus Hiddink (kwenye mashindano yote).
- The Blues kwa sasa ndiyo timu ambayo haijapoteza kwenye mechi nyingi kwenye Premier League (imeshinda mechi 3 na kutoka sare mara 4)
- The Gunners wameshindwa kufunga mfululizo kwa mara kwanza kwenye michezo ya ligi tangu August 2012.
The Gunners are at home to Burnley in the FA Cup next weekend, and the Blues are away at the MK Dons in the same competition.
The Gunners watakuwa ugenini watakapokutana na Burnley kwenye mchezo wa FA Cup wiki ijayo wakati The Blues watakuwa ugenini MK Dons kwenye mchezo wa FA pia.
Vikosi vilivyocheza Arsenal vs Chelsea
Takwimu za mchezo Arsenal vs Chelsea
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment