Kocha Pluijm aunga mkono Niyonzima kutimuliwa Yanga

I
Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm
SIKU moja baada ya Yanga kusitisha mkataba wake na Haruna Niyonzima, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm ameibuka na kusema alikwishamuondoa kiungo huyo kwenye mipango yake.
Pluijm alisema kwamba, anaunga mkono hatua iliyochukuliwa na uongozi, kwa sababu Haruna ameshindwa kujiheshimu kama mchezaji wa kulipwa.
“Sasa naandaa kikosi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na nimekwishamfuta Haruna katika daftari langu la wachezaji”, alisema Pluijm.
Yanga ilivunja mkataba na kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda kwa madai ya mchezaji huyo kukiuka vipengele na anatakiwa kulipa fidia ya dola za Kimarekani 71, 175 hii ikiwa ni kufidia ya gharama ambazo Yanga imeingia katika kumuongezea mkataba mpya ambao unamalizika 2017.
Sakata la kufukuzwa kwa Niyonzima Yanga lilianza mwezi uliopita, baada ya mchezaji huyo kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, Cecafa, nchini Ethiopia na akachelewa kurejea baada ya mashindano hayo.
Baada ya sakata hilo, Yanga ilimsimamisha kwa muda usiojulikana kabla ya suala lake kupelekwa Kamati ya Nidhamu, ambayo imekuja na maamuzi ya kuachana naye.
Niyonzima aliwasilisha vielelezo vyake, lakini taarifa ya Yanga ilisema kuwa kiungo huyo alidanganya ili kukwepa hatua za kinidhamu ndio maana alifunga plasta gumu (PoP) wakati hana jereha baada ya kurejea akiwa amechelewa na vielelezo vingine alivyowasilisha vilikuwa feki.
Haruna alijiunga na Yanga mwaka 2011 akitokea APR ya kwao, ambako aliwasili mwaka 2007 akitokea Rayon aliyoichezea kwa misimu miwili


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: