December 30 Ligi Kuu ya Hispania iliendelea kwa michezo 9 kupigwa katika viwanja mbalimbali, huu ni muendelezo wa mechi za Laliga ambapo ilikuwa imesimama kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya Christmas, hivyo December 30 iliendelea kama kawaida. Miongoni mwa michezo iliyochezwa December 30 ni mechi kati ya FC Barcelona dhidi yaReal Betis.
Huu ni mchezo ambao umechezwa katika uwanja wa Camp Nou wa jiji la Barcelona, huu ni uwanja ambao unatajwa kuwa miongoni mwa viwanja vyenye uwezo wa kubeba mashabiki wengi. Kwa sasa FC Barcelona ambao ni wapinzani wa jadi na Real Madrid, walikuwa wakiombewa dua baya na wapinzani wao hao.
Baada ya Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Real Sociedad katika mchezo wa mapema wengi walikuwa wakisubiri mchezo wa FC Barcelona kuona watafanyaje, hivyo kama Barcelona wangepata matokeo ya sare au kufungwa wangekuwa wamepunguza tofauti ya point dhidi ya wapinzani wao. Hata hivyo FC Barcelona walifanikiwa kubakisha point tatu nyumbani, baada ya kuifunga Real Betismagoli 4-0.
Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Heiko Westermann aliyejifunga dakika ya 29,Lionel Messi dakika ya 33 na kuweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi 500 akiwa naFC Barcelona, goli la tatu na la nne lilifungwa na Luis Suarez dakika ya 46 na 83. Kwa sasa FC Barcelona ambayo imecheza jumla ya mechi 16 inaongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 38.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment