Chelsea vs Man Utd: The Blues Ndio Kiboko Ya United Katika EPL Tangu 1992 – LVG Mnyonge kwa Hiddink

LOUIS VAN GAAL asingependa kuitazama rekodi/takwimu ya timu yake Manchester United dhidi ya Chelsea katika miaka ya hivi karibuni. 
 The Blues wana rekodi nzuri dhidi ya United kuliko timu yoyote ya ligi kuu ya Uingereza.
Na Ikiwa United watapoteza mechi ya leo – itakuwa rekodi yao mbaya kabisa ya matokeo kwa United tangu mwaka 1936 – wakifungwa mechi tano mfululizo.
Kikosi cha Van Gaal tayari kimeshafikia rekodi iliyodumu miaka 54 baada ya kipigo chao kutoka Stoke City kwenye uwanja wa Britannia Stadium jumamosi iliyopita.
Kocha wa Kiholanzi alikaririwa akitoa ishara kwamba anaweza kujiuzulu bila kusubiri kufukuzwa na mabosi wa Old Trafford.
Lakini United tayari wana rekodi ya kupoteza mechi 16 kwa Chelsea tangu mfumo wa Premier League ulipoanza.
Liverpool wameifunga United mara 13, Arsenal 12, Manchester City 11 na Everton 8.
  Ushindi wa kukumbukwa wa Chelsea dhidi ya United – ni ushindi wa 5-0 uliopatikana mwaka 1999 – msimu ambao United walicheza mechi zote kasoro hiyo bila kupoteza, ushindi mwingine ni 3-0 waliopata katika dimba la Old Trafford msimu wa 2001/02.
Chelsea walishinda 1-0 @Stamford Bridge msimu uliopita shukrani kwa goli zuri la Eden Hazard.
  MECHI ZA USHINDI WA CHELSEA KATIKA EPL VS MAN UTD

1993/94: Chelsea 1 Man Utd 0, Man Utd 0-1 Chelsea
1996/97: Man Utd 1 Chelsea 2
1999/00: Chelsea 5 Man Utd 0
2001/02: Man Utd 0 Chelsea 3
2003/04: Chelsea 1 Man Utd 0
2004/05: Chelsea 1 Man Utd 0, Man Utd 1 Chelsea 3
2005/06: Chelsea 3 Man Utd 0
2007/08: Chelsea 2 Man Utd 1
2000/10: Chelsea 1 Man Utd 0, Man Utd 1 Chelsea 2
2010/11: Chelsea 2 Man Utd 1
2012/13: Man Utd 0 Chelsea 1
2013/14: Chelsea 3 Man Utd 1
2014/15: Chelsea 1 Man Utd 0
  MATOKEO YA LOUIS VAN GAAL VS GUUS HIDDINK 
Ikiwa tutaangalia matokeo ya hivi karibuni pia baina ya makocha wawili – pia shilingi inaonyesha itaangukia upande wa Hiddink.
Rekodi zake dhidi ya LVG akiwa kocha wa PSV wakati LVG akiwa AZ Alkmaar zinaonyesha Hiddink amekuwa mbabe dhidi ya mdachi mwenzie.
PSV 2 AZ Alkmaar 0
AZ Alkmaar 1 PSV 2
PSV 3 AZ Alkmaar 0


Ludewa yetu na maendeleo yetu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: