Wanafunzi zaidi ya mia tano wa shule ya msingi Raranya wilayani Rorya mkoani Mara wamelazimika kusimama masomo kwa zaidi ya miezi mitano kutokana na shule hiyo kufungwa kwa kutokuwa na choo.
Uongozi wa shule umetoa maelezo hayo kwa mbunge wa jimbo la Rorya Lameck Airo kufanya ziara ya kushutukiza na kukuta shule hiyo haina wanafunzi zaidi ya wa darasa la nne wanaoendelea na masomo.
Akiongea katika shule ya msingi Raranya ,mwl Magdalena John amekiri kufungwa kwa shule hiyo, huku akisema wananfunzi wanao endelea na masomo ni wa darasa la nne ambao kwa sasa wanatumia choo ya matundu mawili wanayo changia na walimu
Kutokana na adha hiyo ya wananfunzi kukosa masomo kwa zaidi ya miezi mitano mbunge mteule wa jimbo la rorya Lameck Airo katika kutereza baadhi ya ahadi zake wakati wa kampeni ,akalazimika kuchangia shilingi milioni mbili na nusu kwa ajiri ya kukamilisha ujenzi wa choo katika shule hiyo
Mbali na kukamilisha ujenzi wa choo katika shule ya msingi Raranya pia mbunge amechagia ujenzi wa chaoo ya shule ya msingi Nyamasieki , Kyariko na amekamilisha ujezi wa barabara yenye urefu wa km 3 na nusu itokayo katika kijiji cha ya Raranya hadi kijiji cha Bwiri
0 comments:
Post a Comment