Mshambuliaji raia wa Kenya, Paul Kiongera amefurahishwa na uamuzi wa klabu yake ya Simba SC kumrejesha tena katika kikosi chao wakati huu wakiwa wameanza vizuri msimu wa ligi kuu. Simba imemtema mshambulizi ‘butu’ , Msenegal, Pape N’daw na sasa nafasi hiyo inachukuliwa na Kiongera ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili mwaka uliopita.
Majeraha ya goti yalimfanya kufanyiwa operesheni nchini India. Alikaa nje ya uwanja wa miezi zaidi ya 6 na alipopata nafuu alirudishwa kwa mkataba wa mkopo katika klabu yake ya awali nchini kwao Kenya. Simba imeshawishika kumrejesha tena Kiongera ili kusaidiana na washambuliaji waliopo kusaidia upatikanaji wa magoli.
“Nafuraha kubwa kurejea Simba. Ni timu nzuri na wameanza msimu huu vizuri. Narejea kwa sababu nilikuwa na mkataba nao ambao unamalizika mwaka kesho mwezi wa 6. Natumai kufanya kazi na wachezaji wenzangu kuisaidia timu kufanya vizuri. Simba ina wachezaji wazuri ikiwa watafanya vyema, wana hali ya kupambana na Yanga katika ubingwa. Wachezaji wana nafasi kubwa ya kupata ubingwa”, ni maneno ya mchezaji huyo.
Ludewa yetu na maendeleo yetu
0 comments:
Post a Comment